Mbinu za kupata pesa $100 online kwa mwezi na toloka

Posted by:

|

On:

|

Toloka ni tovuti ambayo unaweza kupata pesa kwa kukamilisha kazi rahisi. Kwa mfano, kutathmini maudhui ya kurasa nyingine za mtandao, kuchukua picha, kuhukumu tovuti na kazi nyingine rahisi.

Unaweza kutengeneza zaidi ya dola 100 ($100 =Ksh.14,500 and $100=Tzs.250,000) kwa mwezi kwa urahisi, unapofanya kazi saa 2-3 kwa siku. Ukifanya kazi kwa saa nyingi ndivyo utapata pesa nyingi.

Vile Toloka inavyofanya kazi

 • Jisajili na hapa.
 • Kamilisha seti ya mafunzo ya haraka ili ujifunze jinsi ya kufanya aina fulani ya kazi
 • Chagua kazi unayotaka kufanya kwenye kompyuta yako au kwenye simu yako.
 • Soma maagizo kwa uangalifu na ukamilishe kazi
 • Withdraw pesa zako.

Kujisajili kwa Toloka

 • Enda kwa Toloka.com.
 • Bofya kitufe cha “Start earning money” (kama unatumia desktop). Ikiwa unatumia simu bonyenza tu “Login”.
 • Bonyeza kifungo cha mtandao wa kijamii ambacho unataka kujiandikisha. Ili kuona mitandao yote ya kijamii, bofya “More social networks”.
 • Unda akaunti ya social media ikiwa bado haujajiandikisha kwenye mtandao wa kijamii.
 • Weka nambari ya simu na ubofye “Send Code”. SMS yenye code ya kuthibitisha itatumwa kwa nambari hiyo.
 • Weka code kutoka kwa ujumbe uiotumwa na ubofye “Submit”. Ikiwa hujapokea code au umeingiza code isio sahihi, unaweza kuomba code ingine mpya baada ya dakika moja.
 • Jaza habari zako: jina la kwanza na la mwisho, tarehe ya kuzaliwa, na nchi. Soma “User agreement”, thibitisha kuwa una umri wa miaka 18 au zaidi, na ubofye “Continue”.
 • Baada ya kujisajili, ukurasa wa kazi utafunguliwa. Unaweza kuanza kukamilisha kazi na ulipwe.

Vidokezo vya kupata pesa zaidi kwenye Toloka:

 • Jaribu kupita mafunzo “qualification” kwa zaidi ya alama 80%, na utapa kazi zenye utalipwa pesa nyingi zaidi.
 • Dumisha usahihi wako unapofanya kazi, kwa sababu usahihi wako utakaguliwa.
 • Fanya kazi kwa angalau saa moja hadi mbili kila siku.
 • Fanya kazi mingi zaidi: Kadiri unavyoendelea kufanya kazi nyingi, ndivyo unavyoweza kupata pesa nyingi. Tafuta kazi zinazolingana na ujuzi na mambo yanayokuvutia, na ujaribu kuongeza tija yako.