Raila Amolo Odinga ni mwanasiasa wa Kenya ambaye alikuwa waziri mkuu wa Kenya kuanzia 2008 hadi 2013. Alikuwa Mbunge wa Jimbo la Langata kuanzia 1992 hadi 2013 na amekuwa Kiongozi wa Upinzani nchini Kenya kwa miaka mingi sana.
Raila Odinga pia ni mmoja wa mwanasiasa tajiri zaidi wa Kenya, kwa hisani ya kazi yake ndefu na uwekezaji katika mafuta na gesi, ardhi, viwanda na vinginevyo.
Kuelekea uchaguzi wa 2022, mwanasiasa huyo alisema alikuwa na thamani ya takriban KSh 2 bilioni. Lakini kiuhalisia Raila anakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya KSh 40 bilioni na amejijengea majumba yanayomfaa. Anamiliki nyumba nyingi za kifahari zikiwemo jumba la rangi ya manjano huko Riat Hills huko Kisumu ambayo inaripotiwa kugharimu mamia ya mamilioni.
Hizi hapa ni baadhi ya nyumba za Raila Odinga.
Nyumba za Raila Odinga.
Nyumba ya Karen.
Karen ni mojawapo ya mtaa waa gharama kubwa zaidi kukaa huku Kenya, kwa sababu ya mazingira yake ya utulivu. Wanasiasa wengi wa Kenya wanaishi hapa.
Nyumba ya Raila Odinga huko Karen iko kwenye kipande cha ardhi cha ekari kumi. Ina lango lililo na usalama wa kutosa, ukuta wa mzunguko wenye nyaya za umeme, vyumba kadhaa vya kulala na kupumzika, gym iliyo na vifaa vya kutosha, na bwawa la kuogelea. Jumba hilo la kifahari linakadiriwa kuwa Ksh 300 milioni.
Hizi hapa picha za nyumba ya raila huko Karen.
Nyumba ya Riat, Kisumu
Jumba hili la kifahari limejengwa juu ya Milima ya Riat huko Kisumu. Ina vyumba 10 vya kulala, Jacuzzi, kumbi za mikutano, ukumbi wa michezo na jiko la hali ya juu.
Mnamo Jumatano, Mei 18, 2023. Idah alitoa picha ya kwanza ikionyesha vile ndani iko, imepambwa na dhahabu. Walikuwa mwenyeji wa wajumbe mashuhuri kutoka Umoja wa Afrika, na picha zilionyesha wakishirikiana katika sebule yenye mandhari ya dhahabu.
Nyuma ya Bondo
Hizi ni mkusanyiko wa picha za nyumba ya Raila huko bondo.
Rais wa zamani Uhuru akiweka shada la maua kwenye kaburi la Jaramogi Oginga. Sanamu ya simba iko juu ya kaburi la baba wa Raila Odinga kama jiwe la kaburi.
Sehemu nyingine nyumbani kwa Raila huko bondo ina “Corridors of Fame” inayoonyesha picha za viongozi mashuhuri ulimwenguni akiwemo Thomas Sankara, John F. Kennedy, Martin Luther King, Mahatma Gandhi miongoni mwa wengine.
Familia ya Raila ikimkaribisha raisi mustaafu Uhuru Kenyatta nyumbani huko Bondo Siaya Kaunti.
4 responses to “Nyumba za Raila Odinga”