Nyumba za Uhuru Kenyatta

Posted by:

|

On:

|

,

Uhuru Kenyatta, kwa ukamilifu Uhuru Muigai Kenyatta, ni mfanyabiashara na mwanasiasa wa Kenya ambaye alishikilia nyadhifa kadhaa serikalini kabla ya kuwa rais wa Kenya kutoka 2013 hadi 2022.

Uhuru Kenyatta ni mtoto wa Jomo Kenyatta, rais wa kwanza wa Kenya, Uhuru alilelewa katika familia tajiri na yenye nguvu ya kisiasa.

Hizi ni nyumba ambazo aliyekuwa rais wa Kenya anamiliki.

Nyumba za Uhuru.

Nyumba ya Narok.

Nyumba hii iko katika ranchi ya ekari 1,000 huko Oloolmongi, kaunti ndogo ya Lolgorian huko Trans Mara, inatoa mandhari ya kutazama wanyamapori, ikizingatiwa ukaribu wake na Mara Triangle.

Uhuru alipata mali hiyo mnamo 2020 kutoka kwa Olerein na Kengani Group. Uhuru anafuga mamia ya ng’ombe kwenye hiyo ranchi. Gharama ya ranchi hiyo haikufichuliwa kwa umma, lakini kwa ukubwa na ukaribu wake na Hifadhi ya Taifa ya Maasai Mara, lazima inagharimu mamilioni kadhaa.

Nyumba ya Ichaweri, Kiambu.

Ichaweri ni kijiji kidogo kando ya Barabara ya Kenyatta huko Gatundu Kusini, Kaunti ya Kiambu. Ni nyumbani kwa marais wawili wa Kenya, Uhuru na babake Mzee Jomo Kenyatta.

Ni nyumba kubwa zaidi ya makazi huko Ichaweri, mlango wake wa umbo la U, kando yake una na bendela ya Kenya,pia ulizi umeiwekwa sawasawa.

Nyumba ya Nairobi.

Karibu na Ikulu ya Kenya, jumba la kifahari lililoripotiwa kujengwa chini ya uangalizi wa rais wa zamani mwenyewe.

Ngome hiyo inasemekana kugharimu Ksh700 milioni. Tofauti na nyumba za rais wa zamani ambazo zilifadhiliwa na umma, hii nyumba ya Uhuru inasemekana kufadhiliwa kibinafsi.

Ni jumba la kisasa ambalo linalindwa na vizuizi na teknolojia ya kisasa na usalama wa GSU masaa 24.

Nyumba yenyewe ina madirisha ya kuzuia risasi, ukuta wa zege, uzio wa hali ya juu wa umeme.

Ina mbawa mbili, moja ikiwa na bwawa la kuogelea na nyingine ina sehemu ya helikopta kutua. Ndani ya kiwanja, kuna mzunguko mdogo unaoelekea kwenye barabara kuu.

Wakati wa ujenzi wa jumba hilo, ulioanza mwaka wa 2015, barabara inayoelekea kwenye mlango wake pia ilipanuliwa na kujumuisha njia maalum kwa ajili ya jumba hilo.

Nyumba ya Narok

Uhuru pia anamiliki jumba la kifahari huko Nakuru, ambalo liko katikati ya eneo lake la ekari 4000.

Uhuru alionekana akistarehe katika shamba la Gicheha akiwa na ng’ombe wake na wafanyikazi.

Comments are closed.