Picha za mtoto wa Nandy

Posted by:

|

On:

|

Mtoto wa Nandy

Mwimbaji wa Tanzania Nandy na mumewe rapper Billnass walipokea mtoto wao wa kike mnamo Agosti 2022.

Alipojifungua, Nandy alisema mtoto wake atakuwa chanzo cha furaha yake.

“Nataka kumshukuru Mungu kwa kuwa Yeye ni Mweza, msichana wa Kichaga amezaliwa,” aliandika.

“Nampenda mama yangu kwa sababu sasa naona maana halisi ya kuitwa mama. Sijawahi kuwa na furaha hivi. Nina furaha kutoka ndani ya moyo wangu.”

Kwa mume wake, Nandy alimshukuru kwa kuwa rafiki mkubwa.

Msichana wake mchanga sasa ni balozi wa kampuni ya bima.

Mnamo Julai 2022, Nandy aliapa kutoweka uso, jina na jinsia ya mtoto wake kutoka kwa macho ya umma, aliapa kumlinda mtoto wake kwa kutochapisha au kumfungulia mtoto huyo ukurasa wa mtandao wa kijamii.

Lakini mwimbaji huyo wa Tanzania alifanya jambo la kushangaza, na kubatilisha tamko lake la awali kwamba watumiaji wa mtandao hawatawahi kuona uso wa mtoto wake au kujua jinsia ya mtoto.

Msanii huyo, aliingia kwenye Instagram mnamo Agosti 21, 2023 kuadhimisha siku ya kuzaliwa ya bintiye Kenaya.

Katika chapisho refu, Nandy hakusherehekea tu siku maalum ya bintiye lakini pia alifunua uso wake kwa ulimwengu kwa mara ya kwanza.

Haya ndiyo aliyoandika Nandy wakati wa birthday ya mtoto wake

“Mwanangu Kenaya, siku kama ya leo ndio siku nilipata nguvu ya kukushika mikononi mwangu kwa mara ya kwanza furaha niliyopata nayo haielezeki na wala sijawahi kuipata maishani mwangu tangu nazaliwa,” Nandy aliandika.

“Baba yako amenifundisha mapenzi lakini wewe umenifundisha jinsi ya kuyaishi mapenzi ya dhati.. nakupenda sana na nakuombea ukue kwenye mikono ya Mungu!

“Uwe mtoto wa baraka kwa wengine wakufurahie na kukuombea pia. Mimi na baba yako tunazidi kumuomba Mungu atupe umri mrefu ili tuweze kushuhudia watoto wako na familia yako!” Aliendelea.

Katika chapisho tofauti, mume wa Nandy, Billnas, pia alijiunga katika kusherehekea siku ya kuzaliwa ya binti yake. Alieleza kufurahishwa na kupata mtoto wao kama sehemu ya maisha yao.

“Kwa Majaliwa na baraka zake Mungu amekufanya uwe katika uzao wangu…una kila sababu ya kuufurahia ulimwengu na kumuomba Mungu akuongoze ili siku moja ulimwengu ufurahie uwepo wako katika ulimwengu,” Billnass aliandika.

Akijibu maswali kuhusu kama atamundia mtoto wake akaunti za mitandao ya kijamii, Nandy alidai kwamba angeshiriki tu maelezo kama hayo mtoto wake anapokuwa na umri wa kutosha kuelewa athari za mitandao ya kijamii.

“Kuhusu swala la mtoto, hatakuwa kwenye mitandao ya kijamii. Hakuna mtu atajua jina lake wala jinsia,” Nandy alisema.

Hata hivyo, sio tu kwamba Nandy amefichua sura na jina la bintiye, bali pia ameenda mbali zaidi kwa kutengeneza akaunti ya Instagram ambayo tayari ina wafuasi zaidi ya 20,000.