Zamani za kale, sungura na fisi walipokea barua ya mwaliko wa harusi. Walihitajika kuhudhuria tukio hilo. Sungura aliandaa karanga na kuziweka kwenye mkoba wake, huku fisi akiandaa miogo yake na kuziweka kwenye mkoba wake. Walianza safari yao.
Njiani, sungura alimshawishi fisi kula chakula chake. Sungura alikula chakula cha fisi kidogo kidogo hadi kikamalizika. Waliendelea na safari, wakahisi njaa tena. Fisi alimwomba sungura ampe karanga zake, lakini sungura alikataa akisema karanga zake zina dawa.
Waliendelea na safari, na sungura akapendekeza wabadilishe majina. Sungura alisema ataitwa “Cha Wageni”, na fisi ataitwa “Cha Wote”. Walipofika, wenyeji waliwakaribisha vizuri na kuwapa chakula, wakisema ni cha wageni. Sungura alikula chakula peke yake.
Asubuhi iliyofuata, wenyeji walileta chakula tena, wakisema ni cha wageni. Fisi alisema hata kama ni cha wageni, yeye atakula. Sungura alimpiga fisi kwa mwiko, na fisi akamrudisha kwa kigoda.