Mungu ni Mungu lyri…
 
Notifications
Clear all

Mungu ni Mungu lyrics by Christopher Mwahangila

(@kwamboka)
Trusted Member
Joined: 8 months ago
Posts: 31
Topic starter  

Nabii Elijah, aliwaita manabii wote, wa mungu Baali

Nabii Elijah, aliwaita manabii wote, wa mungu Baali

Lengo la Elijah, ilikuwa ni kumthibitisha Mungu wa kweli ni yupi,

Kati ya mungu wa baali, na Mungu wa mbinguni.

Akawambia watu nikaribieni mimi, akachukua mawe kumi na mbili akaanza kujenga madhabau.

Akaweka kuni juu yake, akaweka sadaka juu yake,

Akachimba mfereji ,akawambia watu mwageni maji mapipa manne,

Wakamwaga maji mara ya kwanza, wakamwaga maji mara ya pili, wakamwaga maji mara ya tatu.

Elijah, akaanza kumuita Mungu, Mungu wa mbinguni, wewe Mungu, wewe Mungu

Mungu wa mbinguni naijulikane kuwa upo,

Wewe Mungu, wewe Mungu,

Mungu wa mbinguni naijulikane kuwa upo

Moto ukashuka ,ukaramba ile sadaka, ukaramba zile kuni, ukaramba na yale mawe,

Ukaramba na yale mavuno, ukaramba na yale maji,

Watu wakasujudu, wakasema huyu ndiye Mungu, anayepaswa kuabudiwa,

Ndiye Mungu ninaye mwimbia Mungu wa Elijah.

Ooh Mungu (Mungu ni Mungu tu),

Ooh Mungu baba (atabaki kuwa Mungu tu),

Huyu Mungu wa mbinguni jamani (Mungu ni Mungu tu),

Huyu Mungu wa Elijah (atabaki kuwa Mungu tu),

Maishani mwako mama yangu wewe (Mungu ni Mungu tu)

Mahali pote unapotembea (atabaki kuwa Mungu tu),

Ata wainuke wamseme vibaya (Mungu ni Mungu tu),

Ata wamkatae mbele yako (atabaki kuwa Mungu tu).

Na wewe ndugu yangu, unayenisikia, unaye nitazama,

Unaona nini mbele yako? Unaona nini mbele yako?

pengine unaona majaribuaujui utafanya nini, we mkaribie Mungu tu,

Pengine unaona magonjwa, haujui utapona lini we mkaribie Mungu tu.

Pengine unaona vita kubwa, haujui utashinda vipi, we mkaribie Mungu tu.

Pengine unaona watesi, haujui utapita vipi, we mkaribie Mungu tu.

Pengine ni jaribu katika ndoa yako, haujui utashinda vipi, we mkaribie Mungu tu.

Hakuna linaloshidikana kwake Mungu

Hakuna linaloshidikana kwake

Hakuna linaloshidikana kwake Mungu

Hakuna linaloshidikana kwake,

Aliyemshindia Elijah,

Katikati manabii wa baali atakushindia na wewe.

Ooh Mungu (Mungu ni Mungu tu),

Ooh Mungu baba (atabaki kuwa Mungu tu),

Huyu Mungu wa mbinguni jamani (Mungu ni Mungu tu),

Huyu Mungu wa Elijah (atabaki kuwa Mungu tu),

Maishani mwako mama yangu wewe (Mungu ni Mungu tu)

Mahali pote unapotembea (atabaki kuwa Mungu tu),

Ata wainuke wamseme vibaya (Mungu ni Mungu tu),

Ata wamkatae mbele yako (atabaki kuwa Mungu tu).

Wanadamu wamekusemea maneno, kwamba hautaweza ,katika jaribu lako,

Wanadamu wamekusemea maneno, kwamba hautashinda katika vita yako,

Kumbe njia za Mungu, sio sawa na za mwanadamu

Njia za Mungu, sio sawa na za mwanadamu

Mipango ya Mungu ,sio sawa na ya mwanadamu,

Akili ya Mungu, sio sawa na ya mwanadamu,

Maneno ya Mungu, sio sawa na ya mwanadamu,

Mawazo ya Mungu, sio sawa na ya mwanadamu,

Kazi ya Mungu, sio sawa na ya mwanadamu,

Sauti ya Mungu ,sio sawa na ya mwanadamu

Aliye mshindia Elijah,

katikati ya manabii wa baali atakushindia na wewe.

Ooh Mungu (Mungu ni Mungu tu),

Ooh Mungu baba (atabaki kuwa Mungu tu),

Huyu Mungu wa mbinguni jamani (Mungu ni Mungu tu),

Huyu Mungu wa Elijah (atabaki kuwa Mungu tu),

Maishani mwako mama yangu wewe (Mungu ni Mungu tu)

Mahali pote unapotembea (atabaki kuwa Mungu tu),

Ata wainuke wamseme vibaya (Mungu ni Mungu tu),

Ata wamkatae mbele yako (atabaki kuwa Mungu tu).

https://mhariri.com/song-lyrics/gospel-lyrics/mungu-ni-mungu-lyrics-na-ujumbe-wa-kujifunza/

Quote