Ni majira ya alfajiri ambapo kijana kwa jina la Zeki alikuwa akijiandaa kwa safari ya kuelekea kijijini kwa babu yake. Aliye kaa kijijini kabisa, sehemu iliyopo msituni, makazi ya babu yake yamejitenga na nyumba nyingine za kijijini hapo, yaani babu yake anaishi mwenyewe eneo hilo, hana majirani.
Zeki alipomaliza kujiandaa alienda steji kwa ajili ya kupanda gari ambalo linaelekea kijijini huko, alipofika stendi kwa bahati nzuri alikuta gari ambalo limebakisha siti moja ya kukaa, hivyo zeki alipanda na safari ikaanza kuelekea kijijini. Huko wakiwa wapo safarini walipita vijiji kadhaa na kuanza kuingia kwenye pori kubwa ambapo ndio kuna barabara ya kufika kijijini huko hivyo konda wa gari aliamulu abiria wote wafunge vioo vya gari kwani sehemu walipofikia ni sehemu hatari kwa wanyama pori na baadhi ya viumbe wengine.
Safari iliendelea hadi wakaanza kukaribia sehemu wanayoenda ilikuwa ni majira ya saa kumi na moja jioni ambapo gari liliwasili kijijini hapo na kuanza kushusha abiria, abiria wote walishuka akiwemo na Zeki ambapo kila mtu alielekea nyumbani kwao hivyo zeki alianza safari na yeye kuelekea nyumbani kwa babu yake ambaye makazi yake yalikuwa yamejitenga na wenzake, umbali wa kutoka kijijini hapo hadi kufika kwa babu yake inachukua muda mrefu takribani masaa mawili hivyo Zeki alianza safari ya kutoka kijijini pale kuelekea kwa babu yake ambapo ilikuwa ni majira ya jioni saa kumi na mbili.
Alitembea pori na pori huku akijaribu kukumbuka njia kwani ni kipindi kirefu tangu alipoenda kwa babu hivyo baadhi ya njia zilikuwa zimebadilika Miti iliota mingi pia majani barabarani yalionekana kuwa mengi hadi kushindwa kupitika hivyo ilim’bidi zeki asafishe njia apate pa kukanyaga, alitembea kwa umbali mrefu lakini alifikia nusu ya safari na ilikuwa ni majira ya usiku saa moja zeki alionekana kuongeza mwendo huku akiwa makini kuangalia kushoto na kulia, baadhi ya sauti za wanyama zilikuwa zinasikika huku wadudu wa porini wakiendelea kutoa milio yao zeki aliendelea na safari yake ingawaje ilionekana kuwa ni mbali sana. Ilipofika saa moja na nusu zeki kwa mbaali alianza kuliona jengo la babu yake ambalo lilikuwa linaangazwa na mwanga wa mbalamwezi hivyo zeki alijipa matumaini ya kufika kwa babu yake akiwa salama salmin.
Zeki aliongeza mwendo ili aweze kufika haraka, lakini kadri alipokuwa akiongeza mwendo nyumba anaona kama inasogea pale ilipokuwa hivyo umbali ulionekana mrefu.
Baada ya zeki kutembea kwa muda mrefu huku akikaribia kufika nyumbani kwa babu yake lakini kadri anavyosogea ndio umbali unaongezeka.
Zeki alichoka kutembea akaamua kusimama huku akitafakari nini afanye ndipo wazo likamjia amuite kwa sauti ya juu babu yake, akaanza kupiga yowe”Babuuuuuuu”, baada ya dakika 3 alioneka mzee akitoka ndani ya hiyo nyumba kisha akaanza kuangaza macho kuangalia sauti inatokea wapi baada ya kubaini upande wa sauti inapotokea akaanza kufanya maajabu ambayo hata zeki hakutegemea ambayo yalimuacha zeki mdomo wazi, mzee yule alichukua maji kwenye kopo ambayo aliyachota kwenye kisima chake kisha akayanyunyizia kwenye majani baada ya sekunde chache mazingira yakaanza kubadilika, majani yote yaliyokuwa kwenye barabara yalitoka na njia ikabaki safi huku manzari ya nyumba ya babu yake yakawa yanafanana na jumba la mfalme, zeki alistaajabu kuona mambo kama yale bila kupoteza muda babu alimchukua na kumpeleka ndani.
Wakiwa wapo mlangoni zeki alipagawa alipo waona wadada wawili warembo (vigoli) kama ilivyokuwa kwa mwanaume yoyote lijali ni lazima angepagawa na wadada hao, babu alimchukua zeki akampeleka ndani na kumuonesha chumba atakacho kitumia kwa kulala kisha baada ya hapo akamchukua kwenda kumtembeza ili aone mazingira yalivyo zeki na babu yake wakaanza kutembea huku babu akimuonesha zeki maeneo ya sehemu hiyo ambayo mengine hayawezi kuonekana kwa macho ya kawaida hivyo mzee huyo alikuwa na dawa ambayo ukiipaka ndio unaona vitu vyote vilivyopo hapo, zeki alipaka hiyo dawa kisha akaanza kuangalia maajabu ya eneo hilo ambapo aliona mto wa maji unaotiririsha maji yanayong’aa kama dhahabu huku mimea ikiwa inang’aa kama almasi kilicho mstaajabisha kikubwa ni kuona wanyama na ndege wanaoongea kama watu alimsikia chura akiwa anacheka huku bata na ndege wengine wakiwa wanapiga stori.
Zeki aliona kama yupo ndotoni kwani anayoyaona hakuamini baada ya masaa kadhaa walitembea hadi kufika kwenye mlima ambao upo kimya sana kiasi kwamba hata milio ya wanyama,ndege au wadudu haisikiki, babu alimsihi zeki asijaribu hata siku moja kuwaza kuupanda huo mlima kwani unahistoria za kutisha sana ingawaje unamirikiwa na huyo mzee, zeki alitahamaki na kumuuliza babu yake kwanini babu tusiupande babu yake alimueleza ya kwamba viumbe wote wasio tii na kufuata sheria basi huko ndio makazi yao yaani ni mfano wa jela au sehemu ya kifungo cha viumbe wa aina hiyo kwani humo ndani utakuta kuna aina tofautitofauti ya viumbe. (Sehemu ya tatu inakuja)