Bendera ya Kenya
Bendera ya Kenya ilibuniwa baada ya Kenya kupata uhuru mwaka wa 1963. Inatokana na bendera ya chama kilichoongoza kupigania uhuru wa Kenya – The Kenya African National Union (KANU)
Bendera ya Kenya ina mistari mitatu ya mlalo: nyeusi, nyekundu na kijani.
Kila rangi ina maana maalum:
- Nyeusi: Inawakilisha watu wa Kenya.
- Nyekundu: Inawakilisha mapambano ya kupata uhuru na damu iliyomwagika.
- Kijani: Inawakilisha ardhi na asili ya nchi ya Kenya.
- Mistari nyeupe iliongezwa baadaye ili kuashiria amani na umoja.
- Pia ina ngao na mikuki, inayoashiria ulinzi wa taifa ya Kenya.
Picha za bendera ya Kenya
Hizi hapa ni picha za bendera ya Kenya




