Maana ya misimu
Misimu ni mgawanyo wa mwaka kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa. Kuna aina nne za misimu:
Mifano ya misimu
Masika (Spring)
Ni msimu wa machipuko pia huitwa machipuko. Ni msimu wa mpito kati ya majira ya kipupwe na kiangazi ambapo tunaona siku inakuwa ndefu, halijoto inaogezeka na mimea inachanua.
Masika Kenya hukuwa miezi ya Machi – Mei.
Kiangazi (Summer)
Majira ya joto. Kiangazi. Kiangazi Kenya hukuwa miezi ya Juni- Oktoba, Januari – Machi
Demani (Autumn)
Ni msimu wa mapukutiko, ni msimu ambao miti hupukuta majani. Demani ni msimu kati ya majira ya kiangazi na kipupwe, wakati hali ya hewa inakuwa baridi na majani kuanguka kutoka kwenye miti. Demani Kenya hukuwa miezi ya Septemba – Oktoba.
Kipupwe (Winter)
Msimu wa baridi na mvua. Kuna misimu miwili ya mvua au kipupwe Kenya: Machi – Mei, Novemba – Desemba.