Historia ya siku za wiki za Kiswahili
Historia ya Kiswahili inaegemea mno kabila ziliokuwa, na zingine bado zinaishi pwani na visiwani ya Afrika ya Mashariki. Wakati wageni wa Kiarabu walipowasili, walileta dini ya Kiislam. Taratibu, desturi, mila, na tamaduni zikabadilika kufuatia uhusiano wa Waarabu na wenyeji. Uhusiano huo uliongezeka hata kufikia hatua ya kutokea ndoa kati ya wageni na wenyeji. Hapo ndipo siku za wiki ziliporatibiwa kulingana na dini ya Kiislam.
Waislamu hufanya ibada siku ya saba ya wiki, Ijumaa. Hivyo, kulingana nao, mosi ni moja na huhesabu mpaka siku ya saba, ambayo ni siku ya Ijumaa na ndiyo siku maalum ya ibada kwao. Kwa Kiswahili, siku ya kwanza ni Jumamosi, “mosi” inamaanisha moja: Jumapili ni siku ya pili, Jumatatu ni siku ya tatu, Jumanne ni siku ya nne, Jumatano ni siku ya tano , Alhamisi ni siku ya sit ana Ijumaa ni siku ya saba.
Kulingana na mpangilio huu wa siku za wiki unaolingana na historia ya Kiswahili, tunapata:
Siku za wiki za Kiswahili
- Jumamosi inamaanisha “siku ya kwanza”.
- Jumapili inamaanisha “siku ya pili”.
- Jumatatu inamaanisha “siku ya tatu”.
- Jumanne inamaanisha “siku ya nne”.
- Jumatano inamaanisha “siku ya tano”.
- Alhamisi inamaanisha “siku ya sita”.
- Ijumaa inamaanisha “siku ya saba”.
Siku za wiki kulingana na kimataifa
Kulingana na kiwango cha kimataifa, Jumatatu ni siku ya kwanza ya juma. Inafuatwa na Jumanne, Jumatano, Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi. Jumapili ni siku ya saba na ya mwisho ya juma.
Ingawa hiki ndicho kiwango cha kimataifa, nchi kadhaa, huchukulia Jumapili kama mwanzo wa juma.
Kulingana na kiwango cha kimataifa
- Jumatatu – Monday – “siku ya kwanza”.
- Jumanne – Tuesday – “siku ya pili”.
- Jumatano – Wednesday – “siku ya tatu”.
- Alhamisi – Thursday – “siku ya nne”.
- Ijumaa – Friday – “siku ya tano”.
- Jumamosi – Saturday – “siku ya sita”.
- Jumapili – Sunday – “siku ya saba”.
Siku za wiki kulingana na biblia
Kulingana na Biblia ya Kiebrania siku za wiki ni:
- Jumapili – Yom rishon- “siku ya kwanza”.
- Jumatatu -Yom shani- “siku ya pili”.
- Jumanne -Yom shlishi- “siku ya tatu”.
- Jumatano -Yom reveci- “nne siku”.
- Alhamisi -Yom khamshi- “siku ya tano”.
- Ijumaa -Yom shishi- “siku ya sita” na cErev shabbat -“mkesha wa Sabato”.
- Jumamosi -Yom ha- “Sabato” – “siku ya saba”.