Hadithi Fupi za Kiswahili

Posted by:

|

On:

|

Hapa chini tumekupa hadithi fupi; hadithi ya hekaya, ya mafunzo na mahaba.

Hadithi za Kiswahili

Hadithi ya Abunuwasi na Sufuria ya Jirani

Abunuwasi alinunua punda, lakini hakuwa na sufuria kubwa ya kumnyweshea maji. Ilimbidi aende kuazima kwa jirani yake, naye akapewa.

Baada ya siku tatu, Abunuwasi aliirudisha sufuria kwa jirani yake huku akiwa ameweka sufuria nyingine ndogo ndani yake. Abunuwasi akamwambia jirani yake kwamba alipokuwa akichukua sufuria ile, ilikuwa na mimba, na sasa ilikuwa imezaa.

Jirani yake alishangaa na kufurahi sana kusikia kuwa sufuria ile ilikuwa imezaa. Siku nyingine tena, Abunuwasi akaenda kuazima sufuria ileile. Jirani yake alimpa sufuria akitumai kwamba ingerudi imezaa tena, lakini sasa siku nyingi zilipita bila sufuria kurejeshwa.

Ndipo jirani yake alipoamua kumfuata Abunuwasi ili arudishwe sufuria yake. Abunuwasi akamwambia, “Samahani jirani, ile sufuria imefariki ilipokuwa ikijifungua!”

“Haiwezekani! Sufuria haiwezi kufa,” jirani yake alilalamika.

“Kila kinachozaa pia hufa!” Abunuwasi akamjibu.

Mwishowe, jirani yake aliambulia patupu na kurudi kwake bila sufuria.

Hadithi ya Meneja na Amina

Amina alikuwa msichana mchanga. Alikuwa mcha Mungu na alikuwa na ndoto ya kuwa mwalimu. Alifanya bidii sana na akafaulu kumaliza chuo kikuu cha Nairobi na kupata shahada ya elimu. Alikuwa na matumaini makubwa ya kupata kazi nzuri na kujitegemea. Hata hivyo, mambo hayakuwa rahisi kama alivyotarajia. Akaanza kuzunguka kwa muda mrefu sana akitafuta kazi ila hakupata. Alikuwa anatuma maombi kwa kila kampuni na shule aliyoweza kupata lakini hakuna aliyemuita kwa usaili. Alikuwa anahangaika sana na kukata tamaa. Akaendelea kuomba Mungu amsaidie na kumfungulia njia.

Siku moja kwa ndoto, sauti ikamwambia, “Mimi ni Mungu, utajaribiwa ila jitahadhari usikubali kuanguka kwa dhambi kwani kutakuwa na adhabu. Lakini ukishinda jaribu, kutakuwa na zawadi.” Amina alistaajabu na kuogopa. Hakujua maana ya maneno hayo. Akaamka na kusali. Lakini hakushughulika sana na lile ndoto. Akaona ni kama ndoto nyingine tu.

Wiki iliyofuata, alipata simu kutoka kwa kampuni moja kubwa nchini. Ilikuwa ni kampuni ya ujenzi na usanifu. Walimwambia kuwa wamepokea maombi yake na wanamtaka aje kwa usaili siku ya kesho. Amina alifurahi sana. Alikuwa na matumaini kuwa hatimaye amepata kazi. Akaenda kwa usaili na kufanya vizuri. Meneja wa kampuni hiyo alimwambia kuwa amevutiwa na wasifu wake na anataka kumpa kazi. Lakini kuna sharti moja. Meneja akawa anatamani kulala na yeye kwa vile alikuwa mrembo na akamwambia wazi wazi kuwa ndio apate kazi lazima akubali walale na yeye.

Amina alishtuka na kuchukizwa. Alikuwa hajawahi fanya kitendo kama hicho na alikuwa anaheshimu mwili wake. Alikuwa anajua kuwa ni dhambi kubwa mbele za Mungu. Alikataa kata kata na kumwambia Meneja kuwa hawezi kufanya hivyo. Meneja akacheka na kumwambia kuwa anapoteza nafasi ya maisha yake. Akamwambia kuwa kama hatakubali, basi asahau kuhusu kazi. Amina alilia na kumwomba Meneja amhurumie. Alikuwa na shida nyingi na alihitaji kazi. Meneja akasema kuwa hiyo ndio njia pekee ya kumsaidia. Amina alifikiria kwa muda. Alikuwa na hamu ya kupata kazi na kujikimu. Alikuwa anahisi kuwa Mungu amemsahau na hajibu maombi yake. Akaamua kujaribu bahati yake na kumwambia Meneja kuwa atakubali. Meneja akafurahi na kumwambia kuwa wataenda hotelini baada ya kazi. Akaandikia mkataba wa kazi na kumpa Amina. Amina akasaini bila kusoma vizuri. Akaajiriwa kazi.

Amina akaanza kufanya kazi katika kampuni hiyo. Alikuwa anapata mshahara mzuri na kujipatia vitu alivyokuwa anatamani. Lakini alikuwa anajuta sana kwa uamuzi wake. Meneja akawa analala na yeye kila atakavyo. Alikuwa anamtumia kama chombo cha starehe na kumdharau. Alikuwa anamwambia kuwa kama atajaribu kumwacha au kumwambia mtu yeyote, atamfuta kazi na kumharibia jina. Amina alikuwa anateseka sana kiroho na kimwili. Alikuwa anajichukia na kujilaumu. Alikuwa anajua kuwa amemkosea Mungu na kujitia doa. Akaacha kusali na kusoma biblia. Akaanza kujitenga na marafiki na ndugu zake. Alikuwa anajiona kama mtu asiye na thamani.

Walivyokuwa wakiendelea, Amina akaanza kusumbuliwa na mwili kwa ajili ya maradhi aina mbali mbali. Alikuwa anapata maumivu makali, vidonda, homa, na kupungua uzito. Mwanzo alipuuza lakini hali yake ikawa mbaya sana. Akaamua kwenda hospitali kuchunguza afya yake. Alipojaribiwa na daktari, akapatikana ameathirika kwa ukimwi. Amina aliposikia habari hiyo, alizimia. Alipozinduka, alilia na kujutia sana. Akasema, “Heri bado singekuwa na kazi lakini jambo hili lisinipate. Ni heri ningemskiliza Mungu kwa lile ndoto.” Alitamani angepata nafasi ya kubadili maisha yake. Lakini ilikuwa kuchelewa sana. Alikuwa amejiharibia maisha yake kwa sababu ya tamaa na kukosa imani.

Alipolala, ndoto lingine likamjia. Sauti ile ile iliyomwongelesha ikamwambia, “Mwanangu, nahuzunika sana. Hukupita jaribu. Na kwa kweli umelipokea adhabu. Kama usingelala na yule Meneja, sasa hivi ningekuwa nimekubariki na maduka mengi nchini. Ungekuwa tajiri mkubwa. Lakini kwa kuwa ulianguka mtihani, utabaki pale ulipo. Na ni kweli nitazidi kukuinua ukiendelea kunitii. Lakini si kama vile ingelikuwa ungepita mtihani.” Sauti iliponyamaza, Amina akafungua macho na kuona jua la alfajiri. Akashukuru Mungu kwa kumwonyesha ukweli. Akaamua kuwa mtu wa kumpendeza Mungu. Akaomba msamaha kwa dhambi zake na kuomba neema yake. Akaamua kumwacha yule Meneja na kujitenga na kazi hiyo. Akaamua kuanza upya maisha yake kwa kutegemea Mungu. Akaamua kushiriki ujumbe wa Mungu kwa wengine waliokuwa katika hali kama yake. Akaamua kuwa mfano wa imani na matumaini kwa wanaoishi na ukimwi. Akaamua kuwa Amina mpya.

Mahaba ya Mwalimu: Hadithi fupi ya kusisimua

Nilitamani muda wa vipindi darasani umalizike ili niweze kutimiza ahadi niliyokuwa naisubiri kwa siku nyingi. Mwalimu alikuwa akifundisha lakini ni kama nilikuwa sielewi wala sisikii alichokuwa anaelezea. Mawazo yangu yote yalikuwa kwa Madam Jesca. Siku hiyo nilijisemea kuwa iwe isiwe lazima nimweleze ukweli na ikibidi siku hiyo hiyo yatimie ninayoyawaza kila kukicha. Madam Jesca alikuwa ni mwalimu aliyekuwa akitufundisha kwa muda tu baada ya kuwa amemaliza kidato cha sita.

Wakati huo sisi tulikuwa kidato cha nne. Somo alilokuwa akitufundisha ni Kiswahili. Hatimaye mwalimu akatoka na baada ya nusu saa nikaondoka kuelekea nyumbani kwa Madam Jesca. Niliingia baada ya kuwa nimegonga hodi. “We Joshua mbona muda wa vipindi hivi we umekuja huku?” aliniuliza huku macho yake yakionyesha mshangao wa waziwazi. Kanga yake aliyovaa ilikuwa imelowana, na hivyo kusababisha niuone mstari wa chupi. Na kama hiyo haitoshi, Madam Jesca alikuwa ana kitu kingine cha ziada. Awali nilidhani nimekifananisha, lakini alipotembea nikahisi ni chenyewe. Aidha alikuwa amevaa cheni na alikuwa ana shanga kadhaa kiunoni.

“Mwalimu nimekuja unifundishe aina za NOMINO.” “Joshua ni lini sasa utaacha vituko, aina za Nomino nyumbani kwangu eeh!” alinikaribia lakini sikurudi nyuma, niliamua kuwa iwe siku hiyo. Siku ya maamuzi yangu! “Madam, kwa hiyo unataka nifeli ama?” Nilimuuliza kwa uchungu. Nikauona uso wake ukipunguza makali ya hasira. “Hebu ni kitu gani huelewi sasa hapa kwenye Nomino?” aliniuliza. Nikatikisa kichwa na kuingiza mtego wangu. Madam mwenyewe hakuwa mkubwa, ni basi tu, yeye alikuwa amenitangulia kieleimu na sasa ni mwalimu wangu.

“Madamu…nitafundishwa nikiwa nimesimama hivi kweli?” nilihoji huku nikitoa tabasamu hafifu sana. Madam akatembea na kuingia ndani, huku akinionyesha ishara ya kumfuata. Nikafanya kama alivyoniambia, nikiwa nyuma yake nikauona utamu halisi wa Madam ambao huwa unajificha katika mavazi yake ya kiuwalimu.

[Itaendelea]