Colors in Swahili
These are common colors in Swahili:
Red – Rangi Nyekundu
White – Rangi Nyeupe
Black – Rangi Nyeusi
Blue – Rangi ya buluu
Sky Blue – Rangi ya samawati
Green – Rangi ya kijani
Brown – Rangi ya kahawia
Yellow – Rangi ya manjano
Gray – Rangi ya kijivu
Pink – Rangi ya waridi
Purple – Rangi ya zambarau
Orange – Rangi ya machungwa
Gold – Rangi ya dhahabu
Silver – Rangi ya kifedha
Examples of colors in Swahili in sentences
- Kama ningekuwa wewe, ningepaka rangi ya buluu. (If I were you, I would paint it blue.)
- Msichana aliyevaa koti la buluu ni binti yangu. (The girl in a blue coat is my daughter.)
- Uso wako unawaka rangi nyekundu. (Your face is red.)
- Timu yetu ilikuwa inavaa mashati mekundu. (Our team were wearing red shirts.)
- Muuguzi amevaa nguo nyeupe. (The nurse is dressed in white.)
- Tuna paka wawili; mmoja ni mweupe na mwingine ni mweusi. (We have two cats; one is white, and the other is black.)
- Tuna mbwa wawili. Mmoja ni mweusi na mwingine ni mweupe. (We have two dogs. One is black and the other is white.)
- Alikuwa amevaa kofia nyeusi. (She was wearing a black hat.)
- Kuna kondoo mweusi katika kila kundi. (There’s a black sheep in every flock.)
- Benki zote zitapigwa rangi ya samawati ili kuvutia watu zaidi. (All banks will be painted sky blue to make them more appealing to the public.)
- Macho yake yanaakisi rangi ya samawati ya asubuhi yenye jua kali na safi. (Her eyes reflect the sky blue of a clear and bright spring morn.)
- Mlima daima ni kijani. (The hill is always green.)
- Tony aliona mashamba ya kijani na vijiji vidogo na tulivu. (Tony saw green fields and small, quiet villages.)
- Alivaa suti ya kahawia. (He wore a brown suit.)
- Alikuwa na nywele za kahawia. (She had brown hair.)
- Kuna waridi la manjano. (There is a yellow rose.)
- Majani yote kwenye mti yaligeuka kuwa ya manjano. (All the leaves on the tree turned yellow.)
- Mtu aliyevaa suti ya kijivu. (The man in grey suit.)
- Nilipata koti la kijivu. (I found a grey coat.)
- Nimeona gauni hilo kwa rangi ya waridi. (I’ve seen that dress in pink.)
- Rangi ni zambarau badala ya waridi. (The color is purple rather than pink.)
- Sweta yake ni ya zambarau. (Her sweater is purple.)
- Soksi zake ni za zambarau. (His socks are purple.)
- Shati linaweza kupatikana likiwa limetiwa rangi ya machungwa. (The shirt can be found dyed orange.)
- Viatu vilikuwa vya machungwa nilipovinunua. (The shoes were orange when I bought them.)
- Rangi ya dhahabu. (Gloden color.)
- Nyumba ilipakwa rangi ya dhahabu. (The house was painted gold.)
- Rangi ya kifedha. (Silver color.)
- Rangi ya gari ni fedha. (The color of the car is silver.)