Habari meaning katika Kiswahili
Habari ina maana nyingi, kulingana na muktadha.
1. Habari ni taarifa inayotolewa kwa watu kuhusu jambo au tukio fulani.
2. Habari ni neno la kujuliana hali au kuamkiana
Mfano: Habari za asubuhi?
Habari in English
Habari in English inaweza kutafsiriwa kama “news” or “information.” Lakini, kwa mara nyingi neno “habari” hutumika kuuliza mtu jinsi anaendelea, au kusalimia mtu.
Hii haba ni ‘habari’ in English – ya kusalimia mtu:
Habari gani? – What’s new?
Habari yako? – How are you?
Habari za asubuhi! – Good morning!
Habari za mchana! – Good afternoon!
Habari za jioni! – Good evening!
Habari gani? – What’s new?
“What’s new?” Jibu lake ni “Not much; you?”.
Habari gani? Jibu lake ni “Nzuri” au “Njema”
Salamu ya “habari gani” hutumika wakati:
1. kama salamu ya kirafiki
Ni salamu isiyo rasmi inayomuuliza mtu mwingine kile ambacho kimetokea hivi karibuni katika maisha yake. Jibu la kawaida linaweza kuwa “Mzuri”.
2. Kufungua mazungumzo
Katika baadhi ya hali, hasa kwa watu unaowafahamu au watu wapya, ukisema “Habari gani?” inaweza kuwa njia rahisi ya kuanzisha mazungumzo.
.
3. Salamu ya haraka
Ni salamu ya haraka na wakati wowote, inayojulikana ambayo haihitaji jibu la kina.
Habari za asubuhi! – Good morning!
“Habari za asubuhi” ni salamu inayotumiwa hasa nyakati za asubuhi, kwa kawaida kuanzia macheo (6 pm) hadi adhuhuri (12 pm). Inachukuliwa kuwa rasmi zaidi na ya heshima.
Habari za asubuhi? Jibu lake ni “njema” au “nzuri”
Good morning? Jibu lake ni “Good morning to you too!”, “Morning!” n.k.
Habari za mchana! – Good afternoon!
Pia unaweza tumia “Habari za kutwa?” Jibu ni “njema” au “nzuri”.
Good afternoon? Jibu ni “Good afternoon to you as well.”, “Afternoon! How’s your day going?” n.k.
Ni salamu ambayo inaweza kutumika wakati wowote wa mchana. Habari za mchana ni njia ya adabu ya kumsalimia mtu na kwamba unakubali uwepo wake na unamheshimu. Mchana kwa kawaida huwa kati ya adhuhuri (12 pm) na machweo (6 pm).
Habari za jioni! – Good evening!
Maneno yanayotumika jioni kama salamu.
Habari za jioni? Jibu lake ni “njema” au “nzuri”
Good evening? Jibu lake ni “Evening!”, “Good evening! How are you doing?”, “Good evening to you as well.” N.k.
3 responses to “Habari in English – Salamu”