Kinyume cha neno baraka

Posted by:

|

On:

|

Baraka ni neema; kheri; mambo yenye kuleta ustawi.

Kinyume cha baraka

Kinyume cha baraka ni: Laana, msiba, taabu, maafa, shida, nk.

Laana ni ukosefu wa baraka za Mungu.

Msiba ni jambo au tukio lenye kumhuzunisha mtu; huzuni, majonzi, jitimai, buka.

Taabu ni dhiki zinzompata mtu katika maisha.

Maafa ni jambo au tukio haribufu lisababishalo hasara.

Shida ni hali inayomsumbua mtu kama vile mashaka, madhila au maudhi.