Kinyume cha neno bidii

Posted by:

|

On:

|

Bidii ni jitihada katika kutekeleza jambo lolote.

Kisawe cha bidii ni juhudi.

Kinyume cha bidii

Kinyume cha bidii ni uvivu, uzembe, ulegevu, ubwete, ukunguni, utepetevu, ajizi, nk.

Uvivu ni hali ya kutopenda au kutotaka kufanya kazi.

Ukunguni ni hali ya kutopenda kazi.

Utepetevu ni hali ya ulegevu na uvivu, hali ya kutotaka kufanya kazi.

Uzembe ni tabia ya mtu kutowajibika.

Ubwete ni hali ya kukosa kuwa na bidii ya kufanya kazi.