Kinyume cha neno kwama

Posted by:

|

On:

|

Kwama ni:

Shindwa kupita mahali au kuendelea kwa mfano gari linaposhikwa na matope.

Shindwa kufanya au kumaliza jambo.

Visawe vya kwama ni nasa, sakama.

Kinyume cha kwama

Kinyume cha kwama ni kwamua, nasua.

Kwamua ni nasua kitu kutoka mahali ambapo kimekwama, kwa mfano gari katika matope, kinyume cha kwama.

Nasua ni fungulia kitu kilichonaswa kutoka mtegoni.