Kinyume cha neno meza

Meza ni:

Pitisha kitu chochote kinacholiwa kooni hadi tumboni.

Meza pia ni samani inayotengenezwa kwa mbao, bati, plastiki au glasi yenye bapa juu ya mguu mmoja, miguu miwili au zaidi ambayo hutumiwa kuandikia, kuchezea au kulia chakula juu yake.

Kinyume cha meza

Kinyume cha meza (kukula) ni: tapika au tema.

Tapika ni kutoa kitu tumboni kupitia mdomoni ambacho kilikuwa kimekwisha kumezwa.

Tema ni toa kitu kinywani kwa mfano mate au makohozi na kukisukuma nje kwa nguvu.

Tanbihi: Hakuna kinyume cha meza ya samani. Hii ni nomino ambayo haina kinyume.

Related Posts