Mgeni ni mtu asitekuwa mwenyeji wa eneo hilo.
Mgeni pia ni mtu aliyealikwa kwenye shughuli maalumu; mgeni wa heshima, mgeni aliyealikwa kusimamia au kufanya shughuli maalumu kwa mfano kuwapa vyeti wahitimu au kufungua mkutano maalumu.
Kinyume cha mgeni
Kinyume cha mgeni ni: Mwenyeji au mkazi.
Mwenyeji ni:
- Mtu aliyezaliwa na kukulia mahali fulani.
- Mtu anayeishi mahali fulani hata hakuzaliwa pale.
- Mtu au nchi ambayo inapokea na kuhudumia wageni kwa mfano katika mkutano au michezo ya kitaifa na kimataifa.
Mkazi ni mtu anayeishi sehemu fulani. Kwa mfano kijiji, mji, nchi na kadhalika.
Kinyume cha mwenyeji
Tumepata kinyume cha mgeni ni mwenyeji, kwa hivyo kinyume cha mwenyeji ni mgeni