Kinyume cha neno pakia

Posted by:

|

On:

|

Pakia ni kuingiza mizigo au watu ndani ya chombo kama vile gari, meli, mkokoteni na kadhalika.

Mfano: Meli yetu ilipofika Mombasa, ilipakia korosho.

Kinyume cha pakia

Kinyume cha pakia ni pakua.

Neno pakua lina maana tofauti, lakini kwa muktadha huu tunalenga pakua ya kushusha mzigo kutoka kwenye chombo cha kusafiria kwa mfano gari, treni, au meli.

Mfano:  Meli yetu ilipofika Mombasa, wafanyakazi walipakua korosho.