Panga ni:
~ jisu kubwa.
~ mahali maalumu pa kufanyia matambiko.
~ weka vitu kwa utaratibu mzuri.
~kaa kwa makubaliano katika nyumba au chumba cha kukodi.
~fanya uhusiano fulani kwa mapatano.
~ kaa kinyumba, kaa ukiwa hawara.
Kinyume cha panga
Kinyume cha panga ni pangua, haribu, vuruga.
Pangua ni kuacha kufuata utaratibu uliokuwapo.
Pangua pia ni haribu kwa makusudi shabaha au lengo fulani.
Mfano: Golikipa alipangua mpira uliopigwa na timu pinzani golini mwake.
Haribu ni fanya kuwa mbovu sababisha isifae, fanya ishindwe kufanya kazi.
Vuruga ni tibua mpango wa kitu.