Raha ni hali ya kufurahia jambo fulani, hali ya kutokuwa na matatizo yoyote.
Mfano: Vijana wanaishi raha mustarehe.
Kinyume cha raha
Kinyume cha raha ni huzuni, uchungu, shida nk.
Huzuni ni
Uchungu ni :
- Ladha anayopata mtu kinywani baada ya kuramba au kula kitu kisicho kitamu kwa mfano kwinini au shubiri.
- Hisia anazopata mtu anapoumia au kuumizwa kwa mfano kujikata, kujigonga, kupoteza kitu au kupatwa na jambo la kutia huzuni kama kufiwa.
- Maumivu anayopata mtu.
Huzuni ni hali ya kutokuwa na furaha.
Shida ni hali inayomsumbua mtu kama vile mashaka, madhila au maudhi.