Tia ni:
Ingiza kitu ndani ya kitu kingine.
Fanya kitu kiwe na sifa fulani.
Kinyume cha tia
Kinyume cha tia ni toa.
Toa ni:
- Ondoa kitu kilicho ndani na kukiweka nje.
- Sababisha jambo kufahamika, kusikika au kueleweka.
Mfano: toa maji, toa harufu, toa habari, toa sauti.
- Punguza idadi ya vitu kama tendo lililo kinyume na kujumlisha katika hesabu,
- -pa mtu kitu.
Mfano: toa ushauri, toa dawa.