Kinyume cha neno tuma

Posted by:

|

On:

|

Tuma ni agiza mtu aende mahali kufanya jambo fulani.

Peleka kitu au mtu kwa mtu au watu fulani.

Kinyume cha tuma

Kinyume cha neno tuma inategemea na maana unayokusudia:

Kinyume chake ni zuia, komesha, achisha, simamisha nk.

Maana ya zuia ni:

Sababisha jambo au kitu kisimame au kisiendelee.

Kataza mtu asifanye jambo.

Shikilia kitu ili kisianguke.

Komesha ni zuia au kataza jambo lisiendelee kufanyika.

Achisha ni simamisha shughuli au tendo fulani lisiendelee.

Simamisha ni zuia jambo lililokuwa likiendelea lisiendelee, zuia kitu kilichokuwa katika mwendo kisiendelee kujongea.