Ukwasi ni hali ya kuwa na mali nyingi sana, utajiri mkubwa. Ukwasi ni kisawe cha utajii.
Utajiri ni hali ya kuwa na mali au fedha nyingi sana. Mali au fedha nyingi alizonazo mtu.
Kinyume cha utajiri/ukwasi
Kinyume cha utajiri au ukwasi ni: umaskini, ufukara, ukata, uchochole, nk.
Uchochole ni hali ya kukosa kuwa na chakula au pesa.
Umaskini ni hali ya kutokuwa na mali.
Ufukara ni kuwa mchochole, maskini aliyepindukia.