Legend in Swahili (English to Swahili Translation)

Definition of legend in English

A traditional story sometimes popularly regarded as historical but not authenticated.

An extremely famous or notorious person, especially in a particular field.

Legend in Swahili

The translation of legend in Swahili depends on the above definitions:

Legend as a story is translated as simulizi, hekaya or ngano.

Legend as a famous person is translated as shujaa, jabari, chagina or jagina.

Examples of legend in Swahili in sentences

  • Tamthilia hiyo ilikuwa imetokana na simulizi za Waluo. (The play was based on Luo legends.)
  • Kwa mujibu wa simulizi (hekaya/ngano), alikimbia kwa kuruka kutoka maporomoko ya maji hadi baharini. (According to legend, he escaped by leaping from the cliffs into the sea.)
  • Alitusimulia hekayasi ya mji wenye mizimu (simulizi/ngano). (He told us the legend of the ghostly town.)
  • Hii ni simulizi maarufu. (This is a popular legend.)
  • Alikuwa shujaa wa wakati wake (jabari/chagina/jagina). (She was a legend in her own lifetime.)
  • Simulizi ya asili yake ya ajabu bado inaendelea. (The legend of his supernatural origins lives on.)
  • Simulizi ina ukweli mwingi. (The legend has much of foundation.)
  • Ni vigumu kutofautisha kati ya simulizi na ukweli. (It is difficult to separate legend from truth.)
  • Tukio hilo limekuwa simulizi ya familia tangu wakati huo. (The incident has since become a family legend.)
  • Matendo yake yamegeuka kuwa simulizi (yameingia hekaya/ngano). (His deeds have passed into legend.)
  • Simulizi hii bado inaenea miongoni mwa watu. (This legend story still spreads among the people.)
  • Muziki wake umemfanya kuwa shujaa anayeishi (jabari/chagina/jagina aliye hai). (His music has made him a living legend.)
  • Kasri limejaa historia na simulizi. (The castle is steeped in history and legend.)
  • Simulizi zinasema kuwa kabila la Wabantu lilitoka msitu wa Kongo. (Legend has it that the Bantu tribe came from Congo forest.)
  • Amekuwa shujaa katika historia ya jeshi. (He has become a legend in the military history.)
  • Simulizi zinasema kwamba Naomi aliuawa kwa kufanya uchawi. (Legend has it that Naomi was put to death for practising witchcraft.)
  • Hadithi ya jinsi alivyookolewa tayari imekuwa simulizi. (The story of how she was rescued has already passed into legend.)
  • Kazi yake ya ujasiri nyuma ya mistari ya adui sasa ni simulizi. (Her daring work behind the enemy lines is now legend.)
Related Posts