Definition of loyal in English
Loyal is giving or showing firm and constant support or allegiance to a person or institution.
Loyal in Swahili
Loyal in Swahili is -aminifu.
Maana ya -aminifu katika Kiswahili
-aminifu ni kutenda jambo vile ulivyoagizwa. (doing what you were instructed to do.)
Examples of loyal in Swahili in sentences
- Sijisikii mwaminifu kwa kampuni hii tena. (I don’t feel loyal to this company any longer.)
- Wamebakia kuwa waaminifu kwa rais. (They had remained loyal to the president.)
- Alikuwa mwaminifu kwa nchi yake. (He was loyal to his country.)
- Jack amekuwa mfanyakazi mwaminifu katika kampuni hii kwa karibu miaka 50. (Jack has been a loyal worker in this company for almost 50 years.)
- Alikuwa mtumishi wa umma mwaminifu, mashuhuri na mwenye uwezo mkubwa. (He was a loyal, distinguished and very competent civil servant.)
- Wanajeshi waaminifu walianzisha mashambulizi ya kukabiliana na waasi. (Loyal armed forces launched a counter-attack against the rebels.)
- Wanajeshi walibaki waaminifu kwa rais. (The troops remained loyal to the president.)
- Zuri alikuwa rafiki yake wa kudumu na mwaminifu. (Zuri was her constant friend and loyal.)
- Yeye ni mwaminifu na anategemewa kabisa. (He is loyal and totally dependable.)
- Ni rafiki mwaminifu.( She is a loyal friend.)
- Daima amebaki mwaminifu kwa kanuni zake za kisiasa. (She has always remained loyal to her political principles.)
- Alibaki mwaminifu kwangu katika hali ngumu na mbaya. (He remained loyal to me through thick and thin.)
- Walikuwa waaminifu bila kuyumbayumba kwa marafiki zao. (They were unflinchingly loyal to their friends.)
- Yeye ni mwaminifu sana kwa marafiki zake. (She’s very loyal to her friends.)
- Ninamhukumu kuwa mwaminifu. (I judge him to be loyal.)
- Watu walibaki waaminifu kwa nchi yao. (The people stayed loyal to their country.)
- Daima amekuwa rafiki mwaminifu kwetu sote. (He’d always been such a loyal friend to us all.)
- Rafiki zake wengine wote walipomwacha, Steve aliendelea kuwa mwaminifu. (When all her other friends deserted her, Steve remained loyal.)
- Yeye ni rafiki yangu mwaminifu. (She’s a loyal friend of mine.)
- Mbwa ni wanyama waaminifu. (Dogs are loyal animals.)