Kikomo ni alama ya uakifishaji inayotumika mwisho wa sentensi. Inaonyesha kwamba sentensi imekamilika na kwamba msomaji anapaswa kuendelea na sentensi inayofuata.
Matumizi ya kikomo
a) Mwishoni mwa sentensi
Huonyesha mwisho wa sentensi.
Mfano
Kioo kimevunjika.
Mtoto ameenda shule.
Mama amepika chakula.
Nitafika nyumbani mapema.
b) Kufupisha maneno.
Mfano
S.L.P. (Sanduku la posta)
Bw. (Bwana)
Mhe. (Mheshimiwa)
U.N.O. Y.C.S. Dkt. N.k.
c) Kuonyesha saa/ muda
Mfano
Misa ilianza saa 4.30 asubuhi.
Saa 12:00.
Tukutane 2.45 alasiri.
d) Katika hesabu, huonyesha isiyo nzima.
Mfano
Ukigawa tatu mara mbili utapata 1.5
10/100 =0.1
e) Kuonyesha senti katika pesa.
Mfano
Bei yake ni shilingi 12.50
Sh 100.00 (shilingi mia moja)
f) Katika kuonyesha kiwango cha kitu
Mfano
Kg 2.5 (kilo mbili na nusu)
L 5.0 (lita tano)