Methali za Kiswahili
Hapa chini tumekupa methali za Kiswahili zaidi ya 400. Tumezipanga kulingana na herufi:
Methali zinazoanza na herufi A
- Ada ya mja hunena muungwana ni kitendo.
- Ada ya mja hunena muungwana ni vitendo.
- Adhabu ya kaburi aijuaye maiti.
- Adhabu ya kaburi, aijuaye maiti.
- Adui wa mtu ni mtu, adui mpende, adui aangukapo mnyanyue.
- Afadhali ya Musa kuliko ya Firauni.
- Afya ni bora kuliko mali.
- Ahadi ni deni.
- Aibu ya maiti aijuaye mwosha.
- Aisifuye mvua imemnyea.
- Alisifuye jua limemwangaza.
- Ajali haina kinga.
- Ajizi ni nyumba ya njaa.
- Akiba halozi, akiba si mbi ijapokuwa ya kumbi, siku ya kivumbi hutiwa motoni.
- Akili ni mali, akili nyingi huondoa maarifa.
- Akili ni nywele kila mtu ana zake.
- Akili nyingi huondoa maarifa.
- Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.
- Akutendaye mtende, mche asiyekutenda.
- Aliye juu mngoje chini.
- Aliye kando haangukiwi na mti.
- Aliyekula kitovu chako hatakuachia utumbo.
- Aliyekunyima kunde/mbaazi amekupungunguzia mashuzi.
- Aliyekunyoa shungi kakupunguzia kuchana.
- Aliyetota hajui kutota.
- Aliyeumawa na nyoka akiona unyasi hushituka.
- Amani haipatikani ila kwa ncha ya upanga.
- Amnyimaye punda adesi ampunguzia mashuzi.
- Anayemwamini Mungu si mtovu.
- Angalipaa juu kipungu kamwe hafiki mbinguni.
- Angurumapo Simba, mcheza nani?
- Asio mali, hasidi wa mwenye mali.
- Asiye na bahati habahatiki.
- Asiye na mwana aeleke jiwe.
- Asiyejua utu si mtu.
- Asiyekubali kushindwa si mshindani.
- Asiyesafiri husifu upishi wa mama yake tu.
- Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
- Atangaye na jua hujua.
- Avumaye baharini papa kumbe wengine wapo.
- Awali ni awali hakuna awali mbovu.
Methali zinazoanza na herufi B
- Baada ya dhiki faraja.
- Baada ya dhiki faraja.
- Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi.
- Balaa hukutia mtu wako.
- Bandu bandu humaliza gogo.
- Bandubandu humala gogo.
- Baniani mbaya kiatu chake dawa.
- Baniani mbaya, kiatu chake dawa.
- Bao nene si chuma chembamba.
- Barua ya moyo husomwa juu ya panda la uso.
- Bendera hufuata upepo.
- Bilashi, bilashi, katu haitoshi.
- Binadamu ni kama kilihafu hakosi uchafu.
- Bura yangu sibadili kwa rehani.
- Bura yangu sibadili kwa rehani.
Methali zinazoanza na herufi C
- Chanda chema huvikwa pete.
- Chelewa chelewa, utakuta mwana si wako.
- Chombo kilichopikiwa samaki hakiachi kunuka vumba.
- Chovya chovya humaliza buyu la asali.
- Chungu kidogo huchemka upesi.
- Chururu si ndondondo.
Methali zinazoanza na herufi D
- Dalili ya mvua ni mawingu.
- Damu ni nzito kuliko maji.
- Dau la mnyonge haliendi joshi likienda joshi ni matakwa ya Mungu.
- Dau la mnyonge haliendi joshi, likienda Mungu kapenda.
- Dawa ya deni kulipa.
- Dawa ya jipu kulipasua.
- Dawa ya moto ni moto.
- Debe shinda haliachi kutika.
- Debe tupu haliachi kuvuma.
- Domo kaya samli kwa mwenye ngombe.
- Dondandugu halina dawa.
- Dua la kuku halimpati mwewe.
- Dunia hadaa ulimwengu shujaa.
Methali zinazoanza na herufi E
- Eda ni ada yenye faida.
Methali zinazoanza na herufi F
- Fadhila mpe mama na Mola atakubariki.
- Fadhila za punda mashuzi.
- Fadhili ukitenda usingoje shukrani.
- Fahari isiyo na ari haina heri.
- Fimbo ya mbali haiuwi nyoka.
- Fumbo mfumbie mjinga mwerevu huling’amua.
- Fumbo mfumbie mjinga, mwerevu ataling’amua.
- Funika kombe mwanaharamu apite.
Methali zinazoanza na herufi G
- Ganda la muwa la jana chungu kaona kivuno.
- Ghururi na binadamu hawaachani.
- Ghushi dhahabu na shaba dhambi na dhawabu havighushiki.
Methali zinazoanza na herufi H
- Haba na haba hujaza kibaba.
- Hadhari kabla ya hatari.
- Hakuna bamvua lisilo usubi.
- Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.
- Hakuna masika yasiyo na mbu.
- Hakuna masika yasiyokuwa na mbu.
- Hakuna ziada mbovu.
- Hamadi kibindo ni silaha iliyo mkononi.
- Hapana maji yasiyo na mawimbi.
- Haraka haraka haina baraka.
- Hasira hasara.
- Hasira ya mkizi furahaya mvuvi.
- Hatua moja hufupisha safari.
- Heri kujikwaa kidole kuliko ulimi.
- Heri mchawi kuliko mtu fitina.
- Heri nusu shari kuliko shari kamili.
- Hewala! si utumwa.
- Hindi ndiko kwenye nguo na wendao uchi wako.
- Huenda umaskini ukakaribia ukafiri.
- Hukutia mtu wako.
Methali zinazoanza na herufi I
- Ibilisi wa mtu ni mtu.
- Ingiwa na shake.
- Inuka twende ni kwa waaganao.
- Ivushayo ni mbovu.
Methali zinazoanza na herufi J
- Jambo la ukucha halichukuliwi shoka.
- Jaribu huleta fanaka.
- Jawabu la kesho andaa leo.
- Jawabu wakatiwe na wakatiwe si zani.
- Jimbi wa shamba hawiki mjini.
- Jino likingoka ukubwani halimei tena.
- Jogoo likiwika lisiwikae kutakucha.
- Jogoo wa shamba hawiki mjini.
Methali zinazoanza na herufi K
- Kafiri akufaaye si Islamu asiyekufaa.
- Kamba hukatikia pabovu.
- Katakata pua uunge wajihi.
- Katiti ni tamu kingi kina kiembeza.
- Kazi mbi si mchezo mwema.
- Kenda fumbata si kumi nenda uje kesho.
- Kichwa cha kuku hakihimili kilemba.
- Kidole kimoja hakivunji chawa.
- Kifo cha wengi harusi.
- Kila mtoto na koja lake.
- Kila mwacha samboye, huenda ali mwanamaji.
- Kila mwamba ngoma,huvutia kwake.
- Kila mwamba ngoma, ngozi huivuta kwake.
- Kila ndege huruka kwa ubawa wake.
- Kilichoingia mjini si haramu.
- Kilimia kikizama kwa jua huzuka kwa mvua, kikizama kwa mvua huzuka kwa jua.
- Kilimia kikizama kwa jua, huibukia kwa mvua.
- Kimya kingi kina mshindo mkuu.
- Kinyozi hajinyoi akinyoa kujikata.
- Kinywa ni jumba la maneno.
- Kipya kinyemi ingawa kidonda.
- Kisebusebu na kiroho ki papo.
- Kitanda usicholala huwajui kunguni wake.
- Kitegwacho kukitega kwataka ubongo.
- Kivuli cha mgude husaidia walio mbali.
- Kujikwaa si kuanguka, bali ni kwenda mbele.
- Kukopa harusi kulipa matanga.
- Kuku havunji yai lake.
- Kuku mgeni zawadi za kunguru.
- Kula kutamu kulima mavune.
- Kula ni vyepesi lakini kulima ngo.
- Kula uhondo kwataka matendo.
- Kulea mimba si kazi kazi kulea mwana.
- Kunguru mwoga hukimbiza bawa lake.
- Kutoa ni moyo si utajiri.
- Kutoa ni moyo usambe ni utajiri.
- Kuvua si kazi kazi ni magawioni.
- Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi.
- Kuzima koleo si mwisho wa uhunzi.
- Kuzima kwa koleo si mwisho wa uhunzi.
- Kwa mwari kwaliwa na kwa kungwi nako huliwa.
- Kwa mwendawazimu kumeingia mlevi.
- Kwa mwoga huenda kicheko na kwa shujaa huenda kilio.
- Kwea iliyo uchungu si uongo ulio mtamu.
- Kwendako mwinyi hurudi mwinyi.
- Kwenye udongo hukosi mfinyanzi.
Methali zinazoanza na herufi L
La kuvunda halina ubani.
La mgambo likilia kuna jambo.
Leo ni leo asemaye kesho ni mwongo.
Lila na fila havitangamani.
Lililompata peku na ungo litampata.
Linalopita hupishwa.
Methali zinazoanza na herufi M
- Mafiga mawili hayainjiki chungu.
- Mafuu hapatilizwi.
- Maisha ni bahati ifumbate.
- Maji ukiyavulia nguo huna budi kuyaoga.
- Maji mafu mvuvi kafu.
- Maji ya nazi hutafuta mvungulio.
- Maji yakimwagika hayazoleki.
- Majuto ni mjukuu huja baada ya kitendo.
- Makuukuu ya mwewe si mapya ya kengewa.
- Mali bila daftari hupotea bila habari.
- Mali ilivunja nguu milima ikalala.
- Mali ya bahili huliwa na mchwa.
- Mama mkwe hafungui mdomo.
- Mambo kangaja huenda yakaja.
- Mashua ya maskini huzama mtoni.
- Maskini hana kinyongo.
- Maskini hana rafiki.
- Maskini haokoti, akiokota huambiwa keba.
- Mavi usiyoyala wayawingiani kuku?
- Mavi ya kale hayanuki.
- Mbio za sakafuni huishia ukingoni.
- Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo.
- Mbwa wa msasi mkali ni wakali pia.
- Mcha Mungu si mtovu.
- Mchagua jembe si mkulima.
- Mchakacho ujao haulengwi na jiwe.
- Mchama ago hanyeli huenda akauya papo.
- Mchawi akifichua mirimo ya wachawi huuawa.
- Mchele mmoja mapishi mbalimbali.
- Mchelea bahari si msafiri.
- Mchelea mwana kulia hulia yeye.
- Mcheza hawi kiwete ngoma yataka matao.
- Mchimba kisima huingia mwenyewe.
- Mchonga mwiko hukimbiza mkono wake.
- Mchovya asali hachovyi mara moja.
- Mchovya asali hachovyi mara moja.
- Mdomo siri ya gunda.
- Meno ya mbwa hayaumani.
- Mfa maji haachi kutapatatapa.
- Mfa maji haishi kutapatapa.
- Mfichauchi hazai.
- Mfinyanzi hulia gaeni.
- Mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
- Mgaagaa na upwa, hali wali mkavu.
- Mganga hajigangi.
- Mgema akisifiwa tembo hulitia maji.
- Mgeni njoo mwenyeji apone.
- Mgomba haushindwi na mkunguwe.
- Mgonjwa haulizwi dawa.
- Miye nyumba ya udongo sihimili vishindo.
- Mkaidi hafaidi hadi siku ya Iddi.
- Mkamia maji hayanywi.
- Mkata hana kinyongo.
- Mkate mkavu wa nyumbani ni bora kuliko nyama ya shuwa ya pengine.
- Mke ni nguo mgomba ni kupalilia.
- Mkokoto wa jembe si bure yao.
- Mkono mtupu haulambwi.
- Mkono mtupu haurambwi.
- Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu.
- Mkuki kwa nguruwe mtamu kwa mwanadamu mchungu.
- Mkulima ni mmoja walaji ni wengi.
- Mkwamba hauzai mzabibu.
- Mkware hajiingilii mwenyewe.
- Mla mbuzi hulipa ngombe.
- Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe.
- Mlimbua nchi ni mwananchi mwenyewe.
- Mnyamaa kadumbu.
- Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.
- Mnyonge hana haki mpaka mwenye nguvu apende.
- Minyonyore haunuki hupendeza mauaye.
- Moja shika si kumi nenda rudi.
- Moja ya mkononi yashida mia ya mbali.
- Mpanda farasi wawili hupasuka msamba.
- Mpenzi hana kinyongo.
- Mpiga ngumi ukuta huumia mkonowe.
- Mrina haogopi nyuki.
- Msafiri kafiri.
- Mshale usio na unyoya hauendi mbali.
- Mshika mawili moja humponyoka.
- Mshika mbili moja humponyoka.
- Mshonaji hachagui nguo.
- Msi chembe wala uta si muwani.
- Msitu ni mpya na komba nao.
- Mstahimilivu hula mbivu.
- Mtafitafi hula samaki, mtulivu hula nyama.
- Mtaka cha mvungu ni sharti ainame.
- Mtaka cha mvunguni sharti ainame.
- Mtaka yote hukosa yote.
- Mtambua ndwele ndiye mganga.
- Mtaratibu humshinda mwenye nguvu.
- Mtashi hana kinyongo, ajapowaswa hakomi.
- Mtembezi hula miguu yake.
- Mteuzi heshi tamaa.
- Mti upigwao mawe ni wenye matunda.
- Mtoto akililia wembe mpe.
- Mtoto musikivu ndiye abarikiwaye.
- Mtoto wa nyoka ni nyoka.
- Muamidi cha ndugu, hufa masikini.
- Mume ni kazi, mke ni nguo.
- Mume wa mama ni baba.
- Mvi usiopambwa vyema huyua.
- Mvumilivu hula mbivu.
- Mvuvi ndiye ajuaye pweza alipo.
- Mwamini Mungu si mtovu.
- Mwana kidonda, mjukuu kovu.
- Mwana maji wa kware kufa maji mazoea.
- Mwana wa mhunzi asiposana hufukuta.
- Mwana wa mhunzi asiposana huvuvia.
- Mwanamaji hutaraji kufa maji.
- Mwanzo wa ngoma ni lele.
- Mwanzo wa mvua ni mawingu.
- Mwenda juu kipungu hafikii mbinguni.
- Mwenda pole hajikwai.
- Mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani.
- Mwenye dada hakosi shemeji.
- Mwenye kelele hana neno.
- Mwenye matende hana paja.
- Mwenye nguvu mpishe.
- Mwenye tende hana paja.
- Mwili wa mwenzio ni kando ya mwilio.
- Mwizi akishikwa husema kaokota.
- Mwosha huoshwa.
- Mwosha huoshwa.
- Mwosha husitiri maiti.
- Mzaha mzaha hutumbuka usaha.
- Mzigo mzito mpe Mnyamwezi aubebe.
- Mzoea kutwaa, kutoa ni bangu.
- Mzoea udalali hawezi kazi ya duka.
- Mzoea vya kunyonga, vya kuchinja hawezi.
- Mzungu wa kula hafundishwi mwana.
Methali zinazoanza na herufi N
- Nahodha hodari haogopi mawimbi.
- Nazi mbovu harabu ya nzima.
- Ncha ikikosa mshale mzima hukosa.
- Ndaro haina neno.
- Ndege mjanja hunaswa kwenye tundu bovu.
- Ndege wasiofahamu ulimbo hunaswa kumi kumi.
- Ndoto njema haihadithiwi.
- Ndovu hashindwi na mkongawe.
- Ndugu chungu, jirani mkungu.
- Neno la mbali ni usiku wa giza.
- Ngalawa isiyo na mirengu haisalimiki.
- Ngoja ngoja yaumiza matumbo.
- Ngoja ngoja yaumiza tumbo.
- Ngozi ivute ili maji.
- Nguo ya kuazima, haisitiri matako.
- Nguo ya kuazima haisitiri maungo.
- Ngombe haelemewi na nunduye.
- Ngombe mwenye tume ndiye achinjwaye.
- Nimekula asali udogoni, utamu ungali gegoni.
- Njaa ya leo ni shibe ya kesho.
- Njia ya mwongo ni fupi.
- Nyani haoni kundule, huliona la mwenziwe.
- Nyota ya mtu kuzimika.
- Nyumba ya mgumba haina kilio.
- Nyumba ya udongo haihimili kishindo.
- Nzi kufa juu ya kidonda si haramu.
Methali zinazoanza na herufi O
- Oto la kuku usilaze kicheche.
- Ondoa dari, uezeke paa.
Methali zinazoanza na herufi P
- Pahala pa itifaki ikirahi haipiti.
- Paka akiondoka panya hujitawala.
- Paka akiondoka panya hujitawala.
- Paka akiondoka panya hutawala. Paka hakubali kulala chali.
- Paka mafuta kwa mgongo wa chupa.
- Palilia mkoche, mnazi wende na nyasi.
- Pambo la jeneza lamfaani mtu? Panapo udhiapenyeza rupia.
- Papo kwa papo kamba hukata jiwe.
- Pato kuu ni la Mungu apaye wawi na wema.
- Pema ijapo pema, ukipema sana si pema tena.
- Pembe za chaki.
- Penye nia pana njia.
- Penye uchafu hapakosi nzi.
- Pilipili usiyoila yakuwashia nini?
- Pilipili iliyo shambani, yakuwashiani?
- Pitapita zake hazininyimi usingizi.
- Polepole ndiyo mwendo.
- Punda haendi ila kwa mikwaju.
Methali zinazoanza na herufi R
- Radhi ni bora kuliko mali.
- Rahisi haihalisi.
Methali zinazoanza na herufi S
- Samaki mkunje angali mbichi, akishakauka hakunjiki.
- Samaki mmoja aki huoza wote wameoza.
- Samaki mmoja aki huoza wote wameoza.
- Shauku huondoa maarifa.
- Sheria ni msumeno hukata huku na huku.
- Sheria ni msumeno hukata mbele na nyuma.
- Shetani wa mtu ni mtu.
- Shibe ni mwana malevya na njaa ni mwana malegeza.
- Shukurani ya punda ni mateke.
- Sikio la kufa halisikii dawa.
- Siku njema huonekana asubuhi.
- Siri ya mtungi aijuaye kata.
- Siri ya kaburi aijuaye maiti.
- Sisimizi hawi ngombe.
- Sitafuga ndwele na waganga tele.
- Subira yavuta heri.
Methali zinazoanza na herufi T
- Taa haachi mwiba awe.
- Tabia ya mtu kupenda mambo ya anasa na starehe.
- Tikiti baya liko shambani mwako.
- Titi la mama li tamu, jingine haliishi hamu.
- Tone na tone huwa mchirizi.
- Tupa jongoo na mti wake.
- Turufu huenda kwa mchezaji.
Methali zinazoanza na herufi U
- Ubaya hatima yake mbaya.
- Ubishi chanzo cha mateto.
- Uchungu wa mwana aujuaye mzazi.
- Udogo wa kimo una mambo.
- Ufukara hufanya mtu awe na udhalili moyoni.
- Uhalifu mwenenzi si wa mkazi milele.
- Uhenga hauambiwi maana.
- Uislamu umemshinda fisi.
- Ujana ni moshi ukienda haurudi.
- Ujanja mwingi mbele giza.
- Ukiiga tembo kunya utapasuka msamba.
- Uking’wafua mnofu ukumbuke na kuguguna mfupa.
- Ukiona ambari na zinduna i papo.
- Ukiona ambari, zinduna ipapo.
- Ukiona vyaelea vimeundwa.
- Ukipenda chongo huita kengeza.
- Ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni.
- Ukitaja nyoka shika kigongo.
- Ukitaka kujua utamu wangoma ingia ucheze.
- Ukitaka kuruka, agana na nyonga.
- Ukitaka riba sikio ziba.
- Ukitenda wema usingoje kulipwa.
- Ukubwa ni jaa.
- Ukubwa wa pua si wingi wa kamasi.
- Ukuukuu wa kamba si upya wa ukambaa.
- Ukweli ukidhihiri uongo hujitenga.
- Ulimi hauna mfupa.
- Ulimwengu ni dhaifu siuoneni sheshe.
- Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
- Upeo wa macho si mwisho wa dunia.
- Ushikwapo shikamana.
- Usiache mbachao kwa msala upitao.
- Usidharau dafu embe ni tunda la msimu.
- Usidharau dafu, embe ni tunda la msimu.
- Usidharau kiserema chalima kuliko jembe zima.
- Usicheze na simba ukamtia mkono kinywani.
- Usigombe na mkwezi, nazi imeliwa na mwezi.
- Usikate ubeleko mtoto kabla hajazaliwa.
- Usimlaumu udobi kaniki ni rangi yake.
- Usimwage mtama kwenye kuku wengi.
- Usinipake mafuta kwa mgongo wa chupa.
- Usinivishe kilemba cha ukoka.
- Usione tanga la nguo ukasahau la myaa.
- Usipoziba ufa utajenga ukuta.
- Utajiri ni kivuli.
- Uuzohali ni nyumba ya njaa.
- Uzuri wa mkakasi ndani kipande cha mti.
- Uzuri wa mkakasi ukilowa maji basi.
Methali zinazoanza na herufi V
- Vita vya panzi, furaha ya kunguru.
- Vundo la kinyesi ni malazi ya paka/bata.
- Vunja dari uezeke paa.
- Methali zinazoanza na herufi W
- Wajua tamu ya ua, sumu wanipeani?
- Wanja wa manga si dawa ya chongo.
- Wapiga mbiu ganjoni utasikiwa na nani?
- Waraka ni nusu ya kuonana.
- Wema hauozi.
- Werevu mwingi mbele giza.
Methali zinazoanza na herufi Y
- Ya Kaizari mpe Kaizari na ya Mungu mpe Mungu.
- Ya mgambo ikilia kuna jambo.
- Ya mkiwa haiiti na ikiita hupapata.
- Ya mkiwa haiiti, na ikiita hupapa.
- Yaliyompata peku na ungo yatampata.
- Yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
- Yaliyopita si uele tugange yajayo.
- Yuajifanya mawele, kujitia mitini, ili aambiwe naye yumo.
Methali zinazoanza na herufi Z
- Zana za vita ni silaha.