Nomino za Kawaida (Nomino za Jumla)
Nomino ni nini?
Nomino ni neno linalotaja jina la kitu, mahali, mnyama, mtu, sifa au wazo. Nomino zinaweza kuwa na umoja (kitu kimoja) au uwingi (vitu vingi).
Nomino za kawaida ni nini?
Nomino za kawaida ni majina ya kawaida yanayotumiwa kurejelea vitu, watu, wanyama, mahali, hali au matendo bila kutaja umahususi wake.
Mifano ya nomino za kawaida:
Watu: mtoto, mama, baba, daktari, mwalimu
Wanyama: mbwa, paka, simba, ng’ombe, kuku
Mahali: nyumba, shule, hospitali, mji, barabara
Vitu: kalamu, kitabu, meza, kiti, gari
Mifano ya nomino za kawaida katika sentensi
Watu:
- Mtoto anacheza na mama.
- Baba anaenda kazini.
- Daktari anatibu mgonjwa.
- Mwalimu anafundisha wanafunzi.
Wanyama:
- Mbwa analinda nyumba.
- Paka anapenda kulala.
- Simba ni mfalme wa wanyama.
- Ng’ombe anatoa maziwa.
- Kuku analia.
Mahali:
- Ninaishi nyumbani.
- Watoto wanasoma shuleni.
- Mgonjwa anapata matibabu hospitalini.
- Mji ni mkubwa.
- Gari linapita barabarani.
Vitu:
- Ninatumia kalamu kuandika.
- Ninasoma kitabu.
- Meza iko jikoni.
- Ninakaa kwenye kiti.
- Gari lina magurudumu manne.