Ngeli ya U-YA huwa na majina ya hali, matendo, na kadhalika. Kiambishi {–u} katika umoja na {–ya} katika wingi hutumika katika upatanisho wake wa kisarufi.
Mfano:
Upishi wake «u»mewavutia.
Mapishi yake «ya»mewavutia.
Miundo ya ngeli ya U-YA.
U-MA: Ugonjwa – magonjwa, upana-mapana, uovu-maovu
Nomino katika ngeli ya U-YA
Ugonjwa-magonjwa
Umbo-maumbo
Uwele-mawele
Unyoya-manyoya
Ubele-mabele
Ubua – mabua
Ubele – mabele
Upishi – mapishi
Ulezi —malezi
Uovu-maovu
Ua – maua
Mfano katika sentensi
- Ugonjwa wa moyo unaweza kusababisha kifo. – Magonjwa ya moyo yanaweza kusababisha kifo.
- Umbo la gari hili ni la kuvutia. – Maumbo ya magari haya ni ya kuvutia.
- Uwele ni ugonjwa. – Mawele ni magonjwa.
- Unyoya wa ndege ni laini. – Manyoya ya ndege ni laini.
- Upishi wa chakula cha kienyeji ni tamu. – Mapishi ya vyakula vya kienyeji ni matamu.