Maana ya shahada katika Kiswahili
Shahada ni cheti apewacho mtu baada ya kuhitimu masomo ya chuo cha elimu ya juu kwa mfano chuo kikuu ili kuthibitisha kwamba amefaulu mitihani yake.
Kisawe cha shahada ni digrii.
Shahada pia ni tamko litolewalo na Waislamu ili kukiri kuwa Mwenyezi Mungu peke yake ndiye wa kuabudiwa, na kwamba Mtume Mohamed (S.A.W) ni mtumishi wake.
Shahada in English
Hapa ni tafsiri ya shahada in English kulingana na kila maana:
Shahada ya digrii in English ni degree. Ufafanuzi wa degree in English ni:
“degree, in education, any of several titles conferred by colleges and universities to indicate the completion of a course of study or the extent of academic achievement.”
Mfano: I graduated with a degree in science – Nilihitimu na shahada ya sayansi.
Shahada ya dini ya Kiislamu in English ni: declaration of faith, testimony, or witness.
Degree (education) in Kiswahili
Degree (education) in Kiswahili ni digrii au shahada