Udogo na ukubwa wa neno mlango

Mlango ni:

  • Watu wa uzawa mmjoja. (Kisawe ni ukoo.)
  • Sehemu moja kati ya sehemu za kitabu ambazo zimegawanywa kulingana na mada zilizojadiliwa katika kitabu.
  • Mlango ni uwazi ulio ukutani unaoruhusu kitu kuingia au kutoka; Uwazi unaoruhusu kuingia au kutoka kwa kitu; Kitu kilichotengenezwa kwa ubao, bati, kioo na kadhalika kwa ajili ya kuziba uwazi ulio ukutani unaoruhusu kitu kuingia au kutoka.

Ukubwa wa neno mlango

Kupata ukubwa wa neno mlango tunazingatia kanununi ya ukubwa wa nomino:

Nomino zilizo na herufi {m} mwanzoni na silabi mbili au zaidi katika mzizi, herufi hiyo hudondoshwa.

Neno mlango linaanza na herufi {m} mwanzoni na lina silabi mbili au zaidi katika mzizi, kwa hivyo tunadondosha herufi {m} na kupata ukubwa wa mlango kama lango.

Udogo wa neno mlango

Kupata udogo wa neno mlango tunaongeza kiambishi {ki} kwa ukubwa wa neno mlango.

Udogo wa mlango unakuwa kilango.

Mfano wa sentensi

Mtu amefungua lango. [Hali ya kawaida.]

Jitu limefungua lango. [Hali ya ukubwa.]

Kijitu kimefungua kilango. [Hali ya udogo.]

Wingi wa udogo na ukubwa wa mlango

Majina ya nomino katika ukubwa huainishwa katika ngeli ya LI-YA. Kupata wingi wa ukubwa tunaongeza kiambishi {ma}.

Majina ya nomino katika udogo huainishwa katika ngeli ya KI-VI. Kupata wingi wa ukubwa tunaongeza kiambishi {vi}.

Mfano

Jitu limefungua lango. [Hali ya ukubwa umoja.]

Majitu yamefungua malango. [Hali ya ukubwa wingi.]

Kijitu kimefungua kilango. [Hali ya udogo umoja.]

Vijitu vimefungua vilango. [Hali ya udogo wingi.]

Related Posts