Mbwa ni mnyama afugwaye na binadamu ambaye hulinda na kumsaidia kuwinda.
Ukubwa wa neno mbwa
Kupata ukubwa wa nomino mbwa, tunazingatia sheria hii ya ukubwa wa nomino:
Nomino zenye herufi {m} mwanzoni na zenye silabi moja katika mzizi, herufi hiyo hudondoshwa na kupachikwa kiambishi {ji}.
Nomino mbwa inaanza na herufi {m} mwanzoni na ina silabi moja katika mzizi, tunadondosha herufi {m} na kupachika herufi {ji}.
Kwa hivyo ukubwa wa mbwa ni jibwa.
Udogo wa neno mbwa
Kupata udogo wa neno mbwa tunaongeza kiambishi {ki} kwa ukubwa wa neno mbwa.
Udogo wa mbwa unakuwa kijibwa.
Mfano
Mbwa anakula. [Hali ya kwaida.]
Jibwa linakula. [Hali ya ukubwa.]
Kijibwa kinakula. [Hali ya udogo.]
Wingi wa udogo na ukubwa wa mbwa
Ukubwa wa mbwa, jibwa, hili neno linachukua ngeli ya {li -ya}, katika sentensi. Kumaanisha {li} katika umoja na {ya} katika wingi. Na pia unapachika kiambishi {ma} kupata wingi wa jibwa.
Majina ya nomino katika udogo huainishwa katika ngeli ya KI-VI. Kupata wingi wa ukubwa tunaongeza kiambishi {vi}.
Kwa mfano:
Jibwa linakula. [Hali ya ukubwa umoja.]
Majibwa yanakula.[Hali ya ukubwa wingi.]
Kijibwa kinakula. [Hali ya udogo umoja.]
Vijibwa vinakula. [Hali ya udogo wingi.]