Udogo na ukubwa wa neno mwanamke

Mwanamke ni mtu wa jinsia ya kike.

Ukubwa wa neno mwanamke

Neno mwanamke limeundwa na nomino mbili mwana na mke.

Kupata ukubwa wa mwanamke tunafuata hii sheria hizi za ukubwa wa nomino:

Nomino zinazoanza kwa kiambishi {mw} kiambishi hicho hudondoshwa na kupachikwa kiambishi {j} .

Neno ‘mwana’ linaanza na kiambishi {mw}, kwa hivyo tunadondosha {mw} na kupachika kiambishi {j}.

Nomino zenye herufi {m} mwanzoni na zenye silabi moja katika mzizi, herufi hiyo hudondoshwa na kupachikwa kiambishi {ji}.

Neno ‘mke’ lina herufi {m} mwanzoni na silabi moja katika mzizi, kwa hivyo tunadondosha herufi {m} na kupachika kiambishi {ji}.

Kwa hivyo ukubwa wa mwanamke ni janajike.

Udogo wa neno mwanamke

Kupata udogo wa neno mwanamke tunaongeza kiambishi {ki} kwa ukubwa wa neno mwanamke.

Udogo wa mwanamke unakuwa kijanakike.

Related Posts