Chati ni mchoro wenye maelezo, takwimu na kadhalika zinazoeleza jambo fulani.
Mfano: Tulipotembelea uwanja wa ndege tulionyeshwa chati ya hali ya hewa.
Chati pia ni masihara. (Kisawe ni mzaha)
Wingi wa chati
Wingi wa chati ni chati.
Neno chati halibadiliki katika wingi bali linapakia vilevile.
Mifano ya umoja na wingi wa chati katika sentensi
- Asilimia ya waliomaliza shule imeonyeshwa kwenye chati. (Asilimia ya waliomaliza shule imeonyeshwa kwenye chati.)
- Nitawasilisha habari kwa kutumia chati. (Tutawasilisha habari kwa kutumia chati.)
- Bandika picha kwenye chati. (Bandika picha kwenye chati.)
- Hii ndiyo albamu iliyokuwa kwenye chati. (Hizo ndizo albamu zilizokuwa kwenye chati.)
- Kila siku jina tofauti liliwekwa kwenye kichwa cha chati. (Kila siku majina tofauti yaliwekwa kwenye vichwa vya chati.)
- Kipengee kimeorodheshwa kwenye upande wa kushoto wa chati. (Vipengee vimeorodheshwa kwenye pande za kushoto za chati.)