Kiti ni kifaa kilichotengenezwa kwa mbao, bati, chuma au plastiki kwa madhumuni ya kukalia.
Wingi wa kiti
Wingi wa kiti ni viti.
Umoja wa kiti
Umoja wa kiti ni kiti.
Mifano ya umoja na wingi wa kiti katika sentensi
Umoja | Wingi |
Nakipenda hicho kiti. | Nivipenda hivyo viti. |
Ako chini ya kiti. | Wako chini ya viti. |
Unaweza kukaa kwenye kiti. | Mnaweza kukaa kwenye viti. |
Kiti hiki kinafanya nini hapa? | Viti hivi vinafanya nini hapa? |
Mvulana alikaa kwenye kiti. | Wavulana walikaa kwenye viti. |
Mbwa yuko kwenye kiti. | Mbwa wako kwenye viti. |
Kiti hakiko karibu na dirisha. | Viti haviko karibu na madirisha. |
Tafadhali ondoa kiti hicho kwa sababu kiko njiani. | Tafadhali ondoa viti hivyo kwa sababu viko njiani. |
Hakuna kiti katika chumba hiki. | Hakuna viti katika vyumba hivi. |
Sanduku hili litatumika kama kiti. | Masanduku hiya yatatumika kama viti. |
Itagharimu nini kukarabati kiti hiki? | Itagharimu nini kukarabati viti hivi? |
Kiti hiki hakijarekebishwa. | Viti hivi havijarekebishwa. |
Kiti hiki kimetengenezwa kwa plastiki. | Viti hivi vimetengenezwa kwa plastiki. |
Kiti hiki kimetengenezwa kwa mbao. | Viti hivi vimetengenezwa kwa mbao. |
Kiti hiki kiko chini sana kwangu. | Viti hivi ni viko chini sana kwetu. |
Kiti hiki ni kizuri sana. | Viti hivi ni vizuri sana. |
Ninahisi raha kabisa ninapoketi kwenye kiti hiki. | Tunahisi raha kabisa tunapoketi kwenye viti hivi. |
Tafadhali keti kwenye kiti hiki. | Tafadhali keti kwenye viti hivi. |
Mhudumu alimsaidia mwanamke huyo na kiti. | Wahudumu waliwasaidia wanawake hao na viti. |
Nikupatie kiti? | Niwapatie viti? |
Nipatie kiti, tafadhali. | Tupatie viti, tafadhali. |
Sogeza kiti karibu na meza. | Sogeza viti karibu na meza. |
Kuna paka kwenye kiti. | Kuna paka kwenye viti. |
Hakikisha kwamba kiti ni imara kabla ya kuketi juu yake. | Hakikisha kwamba viti ni imara kabla ya kuketi juu yake. |
Kiti kimevunjika. | Viti vimevunjika. |
Hapa kuna kiti cha starehe unachoweza kukaa. | Hapa kuna viti vya starehe mnavyoweza kukaa. |
Daftari langu liko kwenye kiti. | Daftari zetu ziko kwenye viti. |
Kiti hiki ni cha nani? | Viti hivi ni vya nani? |
Je, kuna kitabu kwenye kiti? | Je, kuna vitabu kwenye viti? |
Mbwa aliruka juu ya kiti. | Mbwa waliruka juu ya viti. |
Hii ni kiti cha starehe. | Hivi ni viti vya starehe. |
Hakuna kiti cha kukalia. | Hakuna viti vya kukalia. |
Usiegemee kwenye kiti changu. | Msiegemee kwenye viti vyangu. |