Ndege ni:
- Chombo cha kusafiria angani. (Kisawe ni eropleni)
- Kiumbe mwenye mabawa na manyoya anayeruka angani. (Kisawe ni nyuni)
Wingi wa ndege
Wingi wa ndege ni ndege.
Umoja wa ndege
Umoja wa ndege ni ndege.
Mifano ya umoja na wingi wa ndege katika sentensi
Umoja | Wingi |
Ningependa kuwa ndege kuliko samaki. | Tungependa kuwa ndege kuliko samaki. |
Ni vigumu kumpiga risasi ndege anayeruka angani. | Ni vigumu kuwapiga ndege wanaoruka angani. |
Ninaona ndege juu ya paa. | Tunaona ndege juu ya paa. |
Ndege juu ya paa ni kunguru. | Ndege juu ya paa ni kunguru. |
Tuliona ndege kwa mbali. | Tuliona ndege kwa mbali. |
Unamwitaje ndege huyu kwa kiingereza? | Unawaitaje ndege hawa kwa Kiingereza? |
Kama ningekuwa ndege, ningeweza kuruka kwako. | Kama tungekuwa ndege, tungeweza kuruka kwenu. |
Tazama! Kuna ndege kwenye mti huo. | Tazama! Kuna ndege kwenye miti hio. |
Mwindaji alimpiga risasi ndege. | Wawindaji waliwapiga risasi ndege. |
Hakuna mtu aliyemwona ndege akiruka. | Hakuna mtu aliyeona ndege wakiruka. |
Mwindaji alilenga ndege, lakini alikosa. | Wawindaji walilenga ndege, lakini wakakosa. |
Ndege huyo alikuwa mkubwa kama tai. | Ndege hao walikuwa nusu wakubwa kama tai. |
Ndege alitandaza mbawa zake. | Ndege walitandaza mbawa zao. |
Ndege huyo alikuwa amefunikwa na manyoya meupe. | Ndege hao walikuwa wamefunikwa na manyoya meupe. |
Ndege huyo alikuwa saizi ya mwewe. | Ndege hao walikuwa saizi ya mwewe. |
Ndege yuko kwenye kiota chake. | Ndege wako kwenye viota vyao. |
Sijawahi kusafiri kwa ndege. | Hatujawahi kusafiri kwa ndege. |
Ndege inanguruma angani. | Ndege zinanguruma angani. |
Alisafiri na ndege kuenda Zanzibar. | Walisafiri na ndege kuenda Zanzibar. |
Ndege hiyo ilitua katika uwanja wa ndege wa Nairobi. | Ndege hizo zilitua katika uwanja wa ndege wa Nairobi. |
Baba yake alimtengenezea ndege ya mfano. | Baba zao waliwatengenezea ndege za mifano. |
Nilisafiri kwa ndege. | Tulisafiri kwa ndege. |
Alikwenda Mombasa kwa ndege. | Walikwenda Mombasa kwa ndege. |
Babu hajawahi kusafiri kwa ndege. | Babu hajawahi kusafiri kwa ndege. |
Ana ndege yake binafsi. | Wana ndege zao za kibinafsi. |
Ndege hiyo ilikuwa na watu 350. | Ndege hizo zilikuwa na watu 350. |
Nilikuwa nimetengeneza ndege ya mfano. | Tulikuwa tumetengeneza ndege za mfano. |
Ndege itasafiri kwa kasi mara mbili ya sauti. | Ndege zitasafiri kwa kasi mara mbili ya sauti. |
Aliposhuka kutoka kwenye ndege, alipigwa risasi na kufa. | Waliposhuka kutoka kwenye ndege, walipigwa risasi na kufa. |