Umoja na wingi wa sahani

Posted by:

|

On:

|

Sahani ni:

  • Chombo kilicho chenye umbo la duara kisicho na kina kidogo na kinachotumiwa kutilia chakula.
  • Kitu bapa kinachotoa sauti wakati kinapochezwa au kupigwa kwenye gramafoni, rekondi ya miziki.

Visawe vya sahani ni ulio na bunguu.

Wingi wa sahani

Wingi wa sahani ni sahani.

Umoja wa sahani

Umoja wa sahani ni sahani.

Mifano ya umoja na wingi wa sahani katika sentensi

UmojaWingi
Bado kuna chakula kwenye sahani yako.Bado kuna vyakula kwenye sahani zako.
Sahani huwekwa kwenye kabati iliyofungwa.Sahani huwekwa kwenye kabati zilizofungwa.
Alirundika chakula zaidi kwenye sahani yake.Walirundika chakula zaidi kwenye sahani zao.
Kuwa mwangalifu usidondoshe sahani hiyo.Muwe wangalifu msidondoshe sahani hizo.
Kuna vitu vyeupe kwenye sahani hii.Kuna vitu vyeupe kwenye sahani hizi.
Alimwaga biskuti kwenye sahani.Walimwaga biskuti kwenye sahani.
Sahani imefunikwa kwa dhahabu inayometa.Sahani zimefunikwa kwa dhahabu zinazometa.
Aliangusha sahani, na ikavunjika vipande vipande.Waliangusha sahani, na zikavunjika vipande vipande.
Mtoto alimaliza upesi chakula kwenye sahani yake.Watoto walimaliza upesi vyakula kwenye sahani zao.
Alichoma kipande cha nyama kutoka kwenye sahani.Walichoma vipande vya nyama kutoka kwenye sahani.
Aliandika jina langu kwenye sahani.Waliandika majina yetu kwenye sahani.
Jim alichukua keki kutoka kwenye sahani.Jim alichukua keki kutoka kwenye sahani.
Alilamba sahani hadi ikawa safi.Walilamba sahani hadi zikawa safi.
Sahani iligonga sakafu na kuvunjika.Sahani ziligonga sakafu na kuvunjika.
Inafaa kujaribu kuunganisha sahani hii pamoja?Inafaa kujaribu kuunganisha sahani hizi pamoja?
Alipangusa sahani yake kwa kipande cha mkate.Walipangusa sahani zao kwa vipande vya mikate.
Alimrushia sahani na karibu amgonge.Waliwarushia sahani na karibu wawagonge.
Sahani iligonga sakafu, na ikavunjika vipande vidogo.Sahani ziligonga sakafu, na zikavunjika vipande vidogo.