Maana ya wimbi katika Kiswahili
Neno wimbi in Kiswahili lina maana kadhaa:
1. Wimbi ni sauti za ngurumo au nuru zinazosafiri hewani.
Mfano: Mawimbi ya sauti, mawimbi ya nuru.
2. Wimbi ni tuta la maji baharini.
3. Wimbi ni mstari matao wenye alama ya ~.
4. Wimbi ni msukumo mkubwa wa jambo ambao ni mgumu kudhibitika.
Mfano: Jiji limekuwa na wimbi la uhalifu kwa mwezi mzima.
5. Wimbi ni aina ya mtama.
Wimbi in English
Hapa ni tafsiri ya wimbi in English kulingana na kila maana.
1. Wimbi ni sauti za ngurumo au nuru zinazosafiri hewani. – Wimbi in English katika ufafanuzi huu ni waves
Mfano: Mawimbi ya sauti – Sound waves, Mawimbi ya nuru – waves of light
2. Wimbi ni tuta la maji baharini. – Wimbi in English katika ufafanuzi huu ni wave or tide.
Mfano: Mawimbi ya Bahari – Sea waves or sea tides.
3. Wimbi ni mstari matao wenye alama ya ~. – Wimbi in English katika ufafanuzi huu ni tilde (a wavy line (~))
4. Wimbi ni msukumo mkubwa wa jambo ambao ni mgumu kudhibitika. – Wimbi in English katika ufafanuzi huu ni surge, outbreak or upsurge.
Mfano: Wimbi la uhalifu – Upsurge in crime.
5. Wimbi ni aina ya mtama. – Wimbi in English katika ufafanuzi huu ni Finger millet (Eleusine coracana).