Wingi wa kivumishi kionyeshi huu

Posted by:

|

On:

|

Huu ni kivumishi kionyeshi cha ngeli [u-/i-,u-/zi-,u-/ya-] kinachodokeza kuwa kitu kipo karibu na msemaji.

Mfano: Mti huu umekauka.

Wingi wa huu

Wingi wa huu ni: hii, hizi, haya

Mfano katika sentensi

Mti huu umekauka. – Miti hii imekauka.

Mmea huu umeaguka. – Mimea hii imeaguka.

Uyoga huu ni tamu. – Yoga hizi ni tamu.

Ugonjwa huu ni hatari. – Magonjwa haya ni hatari.