Yake ni kivumishi kimilikishi cha nafsi ya tatu katika hali ya umoja
Kiwakilishi cha nafsi ya tatu katika hali ya umoja.
Wingi wa yake
Wingi wa yake ni: zake, zao.
Mifano katika sentensi
Nguo yake inapendeza. – Nguo zake zinapendeza, Nguo zao zinapendeza.
Kalamu yake ni bora kuliko yangu. – Kalamu zake ni bora kuliko zangu, Kalamu zao ni bora kuliko zangu.
Meza yake imevunjika. – Meza zake zimevunjika, Meza zao zimevunjika.
Simu yake imepotea. – Simu zake zimepotea, Simu zao zimepotea.