Maji ni kiowevu kisicho na rangi wala Ladha kinachopatikana kwenye mito, Bahari au maziwa na wakati mwingine hutokana na mvua ambacho viumbe hunwa na watu hupikia, huogea au kufulia.
Wingi wa maji
Maji ni nomino isiyohesabika Hakuna wingi wa maji, hatuwezi kuhesabu maji. Kwa hivyo wingi wa maji ni maji.
Umoja wa maji
Umoja wa maji ni maji.
Mfano katika sentensi
– Maziwa yalitiwa kwa maji. (Maziwa yalitiwa maji.)
– Mhudumu, tafadhali niletee maji. (Wahudumu, tafadhali tuletee maji.)
– Hatuwezi kuishi bila maji hata siku moja. (Hatuwezi kuishi bila maji hata siku moja.)
– Kisima ni mahali ambapo unaweza kupata maji. (Visima ni mahali ambapo mnaweza kupata maji.)
– Hakukuwa na maji kwenye kisima. (Hakukuwa na maji kwenye visima.)
– Ua lilikufa kwa kukosa maji. (Maua yalikufa kwa kukosa maji.)