Safi ni:
Isiyo na uchafu
Mfano: Hakuwa na nguo safi.
Nadhifu, -limbwende.
-ema.
-siokuwa na dukuduku, -siokuwa na tashwishi.
Mfano: Maelezo safi yalitolewa na mzazi wake.
Visawe vya safi ni: mufti, barabara, sahihi, nadhifu n.k.
Wingi wa safi
Wingi wa safi ni safi.
Neno safi halibadiliki katika wingi, safi katika wingi linapaki kuwa safi.
Mfano katika sentensi
- Nguo yake ni safi. (Nguo zao ni safi.)
- Hakuwa na nguo safi. (Hawakuwa na nguo safi.)
- Maelezo safi yalitolewa na mzazi wake. (Maelezo safi yalitolewa na wazazi wao.)
- Alitumia lugha safi kueleza. (Walitumia lugha safi kueleza.)
- Mambo yalimwendea safi alipopata kazi. (Mambo yaliwaendea safi walipopata kazi.)