Maana ya maliasili, malighafi, ujasiriamali, urathi na mifano

Posted by:

|

On:

|

Maliasili (Natural resources)

Maliasili ni nyenzo au vitu vinavyotokea katika asili ambavyo vinaweza kutumiwa kwa kuendeleza uchumi.

Maliasili zimegawanywa katika makundi mawili makuu, ambayo ni:

Maliasili hai: Maliasili hizi ni zile zinazotokana na viumbe hai, kama vile misitu, wanyama, mimea, na maji.

Maliasili zisizo hai: Maliasili hizi ni zile ambazo hazina uhai, kama vile madini, ardhi, na mafuta.

Malighafi (Raw materials)

Malighafi ni nyenzo ya msingi ambayo bidhaa hutengenezwa.

Mifano ya malighafi ni pamoja na chuma, mafuta, mahindi, nafaka, petroli, mbao, plastiki, gesi asilia, makaa ya mawe na madini.

Tofauti kati ya maliasili na malighafi

Maliasili ni nyenzo ambazo zinapatikana kwa asili na havijachakatwa au kubadilishwa na binadamu ilhali malighafi ni vitu ambayo vimetolewa kwenye maliasili na viko tayari kusindikwa au kutengenezwa kuwa bidhaa.

Ujasiriamali (Entrepreneurship)

Ujasiriamali ni mchakato wa kuanzisha biashara, unatumia fedha kwa matumaini ya faida.

Mfano:

Kutoa huduma, Kuuza bidhaa au huduma, Kununua biashara yenye iko tayari, Kuanzisha biashara mpya ndani ya biashara iliyopo, Kuanzisha biashara mpya.

Urathi (Inheritance)

Urathi ni dhana inayoashiria kuendelea kwa kitu kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Urithi wa mali – Baada ya kifo cha mtu, kuna cheti kionyeshacho wosia wa namna mali ya mwendazake yatakavyogawiwa warithi.

Urithi wa ujuzi

  • Mwalimu anaweza kumfundisha mwanafunzi wake jinsi ya kucheza ala ya muziki.
  • Mtaalamu anaweza kumfundisha msaidizi wake jinsi ya kufanya kazi yake.