Maana ya jina abir.i
Abir.i
1. (Kitenzi <sie>) safiri kwa chombo cha majini kutoka upande mmoja wa mto, ziwa au bahari hadi upande mwingine. Kisawe ni vuka.
Mfano: Tuliabiri bahari kwa meli.
2. ingia chombo cha kusafiri k.m. basi, meli, mashua n.k. Mnyambuliko ni: abiria, abirika, abirisha.
Abir.i
1. (Kitenzi <ele>) toa maelezo ya kitu kwa usahihi na kwa kueleweka vyema.
2. eleza jambo litakalotokea kabla ya kutokea kwake. Mnyambuliko wake ni: abiria, abirika, abirisha, abiriwa. Visawe ni: tabiri, bashiri.
Abir.i
(Kitenzi <ele>) pata fundisho kutokana na jambo fulani. Mnyambuliko ni: abiria, abiriana, abirisha.
Visawe vyake ni: makinika, tahadhari.
Abir.i Katika Kiingereza (English Translation)
Abir.i katika Kiingereza inategemea maana unayokusudia:
Cross (a body of water).
Embark . (Ingia chombo cha kusafiri)
Desribe, explain. (Eleza au toa maelezo ya jambo fulani.)
Learn a lesson. (Pata fundisho kutokana na jambo fulani.)