Maana ya neno abudu na English translation

Maana ya neno abudu

1. (Kitenzi <ele>) omba Mungu kufuatana na imani fulani.

Mnyambuliko wake ni: abudia, abudisha, abudiwa.

2. (Kitenzi <ele>) penda kitu au mtu sana. Kisawe ni husudu.

Mnyambuliko wake ni: abudia, abudiana, abudisha, abudiwa.

3. (Nomino katika ngeli ya [a-/wa-]), mtoto wa bandia. Kisawe ni: mwanasesere.

Abudu Katika Kiingereza (English Translation)

Abudu katika Kiingereza inategemea na maana unayokusudia:

Abudu (1)            Worship.

Abudu (2)            Love something or someone very much (Adore).

Abudu (3)            A doll.

Related Posts