Maana ya neno ach.a
1. (Kitenzi) <ele> sita kufanya jambo.
Mfano: Juma ameacha shule.
2. telekeza.
Mfano: Aliwaacha watoto wake nyumbani bila ya chakula.
3. toa maelekezo kuhusu jambo la kufanywa na mtu mwingine wakati unapoondoka mahali.
Mfano: Nilipokwenda kwake sikumkuta lakini niliacha ujumbe. 4. bakiza kitu. Kisawe chake ni saza.
Mfano: Mgeni ameacha chakula kingi.
5. -pa mwanamke talaka, kinyume chake ni taliki.
Mfano: Amemwacha mke wake.
6. ruhusu jambo lifanyike.
Mfano: Si vizuri kumwacha mtoto afanye apendavyo.
7. ondokana na tabia fulani. Kisawe chake ni koma.
Mfano: Acha kuvuta sigara. (nah) acha mkono fariki: Rafiki yetu ametuacha mkono.
Mnyambuliko wa neno acha ni: Achana, achika, achisha, achwa.
Ach.a Katika Kiingereza (English translation)
Ach.a katika Kiingereza ni inategemea na maana unayokusudia:
1. To stop, cease.
2. To leave, abandon, or forsake.
3. To give instructions to someone before leaving. (instruct, direct)
4. To leave something behind. (abandon, forsake)
5. To divorce a woman.
6. To allow something to happen. (permit, authorize)
7. To stop doing something.