Maana ya neno ada
1. (Nomino katika ngeli ya [i-/zi-]), gharama au karo anayolipa mtu ili apatiwe huduma fulani k.m. katika elimu, burudani au kupata uanachama katika chama
2. mila au desturi za jamii fulani.
Mfano: Kila kabila lina ada zake za maziko.
3. kawaida katika kufanya jambo.
Mfano: Kunywa chai kila jioni ni ada kwake.
(Methali) Ada ya mja hunena, muungwana ni kitendo.
Ada Katika Kiingereza (English translation)
Ada katika Kiingereza inategemea muktadha:
Ada ya gharama au karo ni: Fee, charge.
Ada ya mila na desturi ni: Culture, tradition.
Ada ya kawaida ni: Habit.