Maana ya neno adhibu na English translation

Maana ya neno adhibu

Matamshi: /aðibu/

(Kitenzi elekezi)

Maana:

1. patiliza, gandamiza au tesa mtu kama vile kumpa kifungo cha jela au kwa kumlazimu atende jambo asilotaka kulifanya.

2. lipiza au toa hukumu au faini ili kufidia makosa aliyofanya mtu.

3. kera au sumbua. Mnyambuliko wake ni: → adhibia, adhibiana, adhibika, adhibisha, adhibiwa.

4. timu kuishinda nyingine hasa kwa mabao mengi.

Adhibu Katika Kiingereza (English translation)

Adhibu katika Kiingereza inategemea maana unayokusudia.

Adhibu ya gandamiza na toa hukumu ni: punish, chastise, discipline.

Adhibu ya kera au sumbua ni: annoy, disturb.

Adhibu ya timu kuishinda na mabao mengi ni: beat, win etc.

Related Posts