Maana ya neno afu na English translation

Maana ya neno afu

Matamshi: /afu/

Nomino katika ngeli ya [li-ya])

Wingi wa afu ni maafu.

Afu 1

Maana: ua la mti wa mwafu ambalo hutumiwa kutengeneza manukato. Kisawe chake ni asumini pori.

Afu 2

(Kitenzi si elekezi)

1. omba Mungu akusamehe, akurehemu au akuokoe kutokana na majanga fulani.

2. ponya.

3. ondosha katika hatari.

Mnyambuliko wa neno afu → afia, afika, afisha.

Afu 3

Nomino katika ngeli ya [li-ya])

Maana: msamaha kutoka kwa Mola.

Afu Katika Kiingereza (English translation)

Afu katika Kiingereza inategemea maana unayokusudia:

Afu 1: blossoms of the wild jasmine used for perfume.

Afu 2: 1. ask for pardon, mercy or salvation from God. 2. cure. 3. save, deliver, pardon.

Afu 3: God’s forgiveness.

Related Posts